TANGAZO


Monday, July 15, 2013

Mjumbe wa Marekani ziarani Misri



Naibu waziri mkuu wa Mambo ya nje Marekni William Burns
Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani William Burns amewasili mjini Cairo Misri tayari kwa mkutano na viongozi wa serikali ya mpito wanaoungwa mkono na jeshi.
Ni Ziara ya kwanza kufanywa na afisaa mkuu wa Marekani tangu jeshi kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohamed Morsi tarehe 4 Julai.
Duru kutoka Ikulu ya rais Marekani, zinasema kuwa Burns atashinikiza kumalizwa kwa ghasia na vurugu na kuundwa kwa serikali ya pamoja ya viongozi wa kiraia watakaochaguliwa kidemokrasia
Awali mwendesha mkuu wa mashtaka alipiga tanji mali za viongozi 14 wa kiisilamu.
Kiongozi wa chama cha Muslim Brotherhood Mohammed Badie na naibu wake Khairat al-Shater wanaripotiwa kuwa miongoni mwa waliokamatwa.
Hatua hiyo ni sehemu ya uchunguzi kuhusu madai ya uchochezi, yaliosababisha ghasia za kisiasa nchini humo.
Mamia ya watu wamefariki wakati wa maandamano yaliyofanywa na mahasimu wa kisiasa kati ya wale wanaomuunga mkono Morsi na wapinzani wake, katika wiki mbili zilizopita.
Wakati huohuo maafisa wanasema kuwa washukiwa wa chama cha Brotherhood, wameshambulia basi lililokuwa linawabeba wafnyakazi wa kiwandani Kaskazini mwa Sinai huku wakiwaua watu watatu.

No comments:

Post a Comment