TANGAZO


Wednesday, July 10, 2013

Malta yasitisha kuwafurusha wahamiaji


Mhamiaji wa Kiafrika
Maafisa wa Kisiwa cha Malta wamesimamisha ndege iliyotayarishwa kuwasafirisha wahamiaji haramu hadi Libya baada ya Mahakama ya haki za binadamu ya Muungano wa Ulaya kuingilia kati.
Utawala wa Kisiwa hicho ulipanga kuwarejesha wahamiaji hao ambao waliwasili eneo hilo wakitumia mtumbwi.Waziri Mkuu Joseph Muscat amesema kwamba wahamiaji 40 wamewasili kisiwa hicho katika kipindi cha wiki moja.Kisiwa cha Malta kiliomba msaada kukabiliana na idadi kubwa ya wahamiaji wanaoendelea kuingia eneo hilo.
Wiki jana wahamiaji 291 waliokolewa baada ya mtumbwi walimokua ndani kwenda mrama. Inaaminika mtumbwi huo uliwasili kutoka Libya na wahamiaji wengi wakiwa raia wa Eriterea.Katika msimu wa jua wahamiaji wengi wa Kiafrika huwasili katika visiwa vya Malta na Lampedusa wakijaribu kuingia Bara Ulaya.
Mahakama ya Ulaya ilitoa amri kusimamisha hatua ya kuwarejesha Afrika wahamiaji haramu waliokua Malta. Hii ilifuatia ombi la dharura kutoka kwa makundi ya kijamii.
Kamishina wa masuala ya ndani wa Muungano wa Ulaya Cecilia Malmstroem amesisitiza kwamba wahamiaji wa kiafrika wanaowasili katika maeneo ya Ulaya wana haki ya kuomba hifadhi.

No comments:

Post a Comment