TANGAZO


Thursday, June 27, 2013

Vodacom Tantrade waungana kunogesha maonesho ya 37 ya DITF


Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, akionesha simu na modem za intaneti ambazo kampuni hiyo, iliikabidhi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam leo. Vifaa hivyo pamoja na udhamini wa maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya mwaka huu ambapo thamani yake ni zaidi ya Shilingi milioni 170. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi. Jacqueline Maleko. (Na zote Mpiga Picha Wetu).
Meneja wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, akikabidhi mfano wa hundi ya Sh. milioni 20 kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi. Jacqueline Maleko, kwa ajili ya kusaidia Mamlaka hiyo, kufanikisha maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (37th DITF). Vodacom imekabidhi simu na modem za intaneti katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Vifaa hivyo pamoja na udhamini kwenye maonesho hayo, vina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 170.
Meneja wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, akikabidhi simu aina ya Smasung Galaxy, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bi. Jacqueline Maleko,  kwa ajili ya kuwawezesha Wakurugenzi na wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TanTrade). Vodacom ilikabidhi simu za aina ya Samsung, modem za intaneti na T-shirt ambazo kampuni hiyo, iliikabidhi katika hafla iliyofanyika leo, kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo, zilizopo kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo pamoja na udhamini wa maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya mwaka huu, vina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 170.
Meneja wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, akikabidhi T-shirt kwa ajili ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TanTrade), kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bi. Jacqueline Maleko. Vodacom ilikabidhi simu za aina ya Samsung na modem za intaneti ambazo kampuni hiyo iliikabidhi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TanTrade), katika hafla iliyofanyika leo, kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo, zilizopo kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo pamoja na udhamini wa maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya mwaka huu vina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 170.

Na Mwandishi wetu
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeingia katika ushirikiano na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu, Vodacom Tanzania kama mdhamini mkuu wa mawasiliano na matangazo kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya  Dar es Salaam  (37th DITF)  yalioanza leo, tarehe 28 Juni na yataendelea hadi 8 Julai 2013 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi. Jacqueline Maleko, ameishukuru Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa hatua yake ya kuitikia mwito wa kudhamini Maonesho hayo kwa mara nyingine na kusisitiza kuwa Kampuni hiyo imekuwa ni kielelezo tosha cha ubora wa huduma za mawasiliano kwa ujumla.

“Tunaishukuru Kampuni ya Vodacom kwa mwito wake wa kuendelea kudhamini maonesho haya kwenye sekta ya Mawasiliano na Matangazo. Hiki ni kielelezo tosha cha ubora wake wa huduma kwa watanzania,” alisema Bi. Maleko.
Maonesho hayo ambayo yanaanza leo tarehe 28 Juni na kuhitimishwa Julai 8 mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya ‘Tanua Wigo wa Biashara yako’ (Expand your Business Horizon).

“Kauli mbiu hii imechaguliwa kutumika kama jukwaa la kutanua wigo wa biashara na kuleta maendeleo endelevu katika ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara kama sera ya taifa inavyoelkeza,” alisema.

Tayari nchi 32 zimethibitisha kushiriki katika maonesho hayo ambapo kampuni za kigeni 400, makampuni ya ndani 1,600 pamoja na Wizara na Taasisi za Serikali 70.

Aidha, kuhusu zoezi la kuchagua banda bora, alisema kuwa litafanyika kati ya tarehe 29 hadi 30 Juni, 2013 chini ya kampuni ya Innovex Development Consulting Ltd ya Dra es Salaam.

TanTrade imetangaza viingilio vya Maonesho hayo kwa watu na magari katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (37th DITF) ambapo kiingilio kwa watu wazima ni Shilingi 2,500 na Shillingi 500 kwa watoto kila siku. Hata hivyo, kiingilio kwa siku maalum ya tarehe 7 vitakuwa ni Shilingi 3,000 kwa watu wazima na watoto Shilingi 1000.

Ada ya maegesho kwa wenye magari madogo katika maonesho hayo ni Shilingi 4,000 kwa maegesho yalitotengwa, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kuingiza magari kama malori na magari makubwa kwa ajili ya huduma nyingine, ambayo yataruhusiwa kuingia usiku kuanzia saa 4.00 kila siku.

Kwa upande wake, Meneja mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, alisema kuwa kampuni yake inajisikia fahari kwa kuingia ubia huu na TanTrade na kuwa mdhamini mkuu katika  sekta ya mawasiliano na matangazo kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Rukia, alibainisha kuwa Vodacom Tanzania inajitahidi kutoa huduma na bidhaa ambazo ni rahisi na nafuu kwa wateja wote nchini.
Katika miaka 37 iliyopita, maonyesho hayo yamekuwa muhimu na kivutio kikubwa nchini Tanzania na nchi za jirani, sambamba na ushiriki wa makampuni ya kimataifa, wizara, idara mbali mbali za serikali, wajasiriamali wadogo, kati na wakubwa toka nchi mbali mbali Duniani ikiwemo za Mashariki, Kusini na Magharibi mwa bara la Afrika, Ulaya na Asia wamekuwa wakiongezeka.
Maonesho hayo ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam yanaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za viwango  vya kimataifa vya biashara vilivyowekwa na Chama cha Maonyesho ya Viwanda Duniani (UFI).

No comments:

Post a Comment