TANGAZO


Thursday, June 20, 2013

Mdahalo wa Uimarishaji Sekta ya Kilimo Halmashauri ya Mkuranga, mkoani Pwani wafanyika

Washiriki wa Mdahalo wa Uimarishaji Sekta ya Kilimo katika Halmashauri ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakiangalia dondoo za mdahalo huo, kabla ya kuanza Wilayani Mkuranga leo. Mdahalo huo umeandaliwa na Taasisi ya Policy Curiosity Society (POCUSO) na kuwashirikisha baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo, Kata, Vitongoji na Vijiji pia baadhi ya wakulima wa Wilaya hiyo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-bayana.blogspot.com)
Mratibu wa Mtandao wa Asasi Wilaya ya Mkuranga (MKUNGONET), Mohammed Katundu, akiwasilisha mada kuhusu Kwa nini tufuatilie Matumizi ya Rasilimali za Umma na Wajibu wa Jamii, wakati wa mdahalo huo, Mkuranga, mkoani Pwani leo.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mdahalo huo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimabali muhimu yapasayo kujadiliwa kwenye mdahalo huo wa kuimarisha sekta ya Kilimo, Halmashauri ya Mkuranga, mkoani Pwani.
Mshiriki wa mdahalo wa uimarishaji sekta ya kilimo katika Halmashauri ya Mkuranga, mkoani Pwani, mkulima Rashid Ibrahim, mkazi wa Mwalusamba, akitoa mchango wake katika mdahalo, uliofanyika Mkuranga leo, ulioandaliwa na Taasisi ya Policy Curiosity Society (POCUSO) na kuwashirikisha baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo, Kata, Vitongoji na Vijiji pia na baadhi ya wakulima wilayani humo.

Mwenyekiti wa Taasisi Policy Curiosity Society (POCUSO), Said Gwaja, akitoa ufafanuzi wakati wa mdahalo wa uimarishaji sekta ya kilimo katika Halmashauri ya Mkuranga, mkoani Pwani leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa mdahalo huo, Shukuru Ngweshani na katikati ni Mwenyekiti wa taasisi ya POCUSO, waandaaji wa mdahalo huo, Abdallah Mikoroti.
Baadhi ya washiriki wa Mdahalo wa Uimarishaji Sekta ya Kilimo katika Halmashauri ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi Policy Curiosity Society (POCUSO), Said Gwaja, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwenye mdahalo huo, kabla ya kuanza wilayani Mkuranga leo. Mdahalo huo umeandaliwa na Taasisi ya Policy Curiosity Society (POCUSO) na kuwashirikisha baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo, Kata, Vitongoji na Vijiji pia baadhi ya wakulima wa Wilaya hiyo.
Washiriki wa Mdahalo wa Uimarishaji Sekta ya Kilimo katika Halmashauri ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakipitia na kufanya masahihisho kwenye taarifa mbalimbali kabla ya kuanza wilayani Mkuranga leo. Mdahalo huo umeandaliwa na Taasisi ya Policy Curiosity Society (POCUSO) na kuwashirikisha baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo, Kata, Vitongoji na Vijiji pia baadhi ya wakulima wa Wilaya hiyo.

Baadhi ya washiriki wa Mdahalo wa Uimarishaji Sekta ya Kilimo katika Halmashauri ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakiwa katika  mdahalo huo, wakipitia makabrasha mbalimbali waliyogawiwa. Mdahalo huo umeandaliwa na Taasisi ya Policy Curiosity Society (POCUSO) na kuwashirikisha baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo, Kata, Vitongoji na Vijiji pia baadhi ya wakulima wa Wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment