TANGAZO


Thursday, June 20, 2013

Maisha jela kwa muuaji wa Rwanda, Sweden


Mahakama moja nchini Sweden imemhukumu maisha jela mtu mmoja kutoka Rwanda kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari yaliyowaacha maelfu ya watu wakiwa wamefariki.
Mahakama hio iliyoko mjini Stockholm ilielezwa kuwa mtu huyo anayefahamika kwa jina Stanislas Mbanenande, ambaye sasa ni raia wa Sweden alishiriki katika mauaji ya watu kadhaa hasa kutoka jamii ya Wa Tutsi kati Mwezi Aprili na Juni mwaka wa 1994.
Mtu huyo pia alipatikana na hatia ya kuongoza kundi la watu wa jamii ya Wahutu wenye msimamo mkali.
Awali majaji kutoka Sweden walisafiri hadi nchini Rwanda ili kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya waathiriwa.

No comments:

Post a Comment