TANGAZO


Friday, June 28, 2013

Kiongozi mkuu wa Al Shabaab 'akataa kujisalimisha'


Kiongozi wa alshabaab Dahir Aweyes
Mmoja wa viongozi wakuu wa al-Shabab nchini Somalia, Sheikh Hassan Dahir Aweys,amekata kujisalimisha , kulingana na taarifa za viongozi vya kiukoo kwa BBC.
Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa bwana Aweys alijisalimisha kwa maafisa wa usalama nchini Somalia baada ya kutofautiana na kiongozi mkuu wa Al shabaab.
Lakini Aweys yuko eneo la Galmudug akiwa na wapiganaji wake baada ya kuPewa idhini ya kuingia katika eneo hilo na maafisa wa utawala.
Walikwenda huko kutoka Mogadishu kuona ikiwa kweli yuko tayari kwa amani.
Aweys anaonekana kama kiongozi mkongwe wa Al Shabaab na yuko kwenye orodha ya Marekani ya washukiwa wa ugaidi baada ya kuhusishwa na shambulizi la kigaidi la 9/11 mwaka 2001 .
Habari za kujisalimisha kwa Aweyes ni ishara kubwa kuonyesha kuwepo mgawanyiko katika uongozi wa Al-Shabaab.
Wiki moja kabla ya kuwasili kwake mjini Adado kupitia baharini, kulikuwa na ripoti kuwa mapigano yalitokea eneo la Baraawe, moja ya ngome kubwa za Al-Shabaab,ambako Aweys alikuwa anaishi.
Ingawa anajikuta katika mazingira asiyoyafahamu vyema, kiongozi huyo anaonekana kuchangayikiwa.
Aliwaambia viongozi wa kikoo waliokwenda kuongea naye kuwa yeye hajajisalimisha na kuwa hayuko tayari kusafiri kwenda Mogadishu.
Bwana Aweyes amekuwa akijulikana na UN kama kiongozi mkubwa katika kundi la al-Shabab na Marekani inamfahamu kama gaidi.

No comments:

Post a Comment