Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu, jijini Dar es Salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7 na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014. (Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO)
Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu, jijini Dar es Salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
Wachezaji wa Timu ya Taifa Stars wakipata chakula walichoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, jijini Dar es Salaam leo, alipokutana nao kuwatakia ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco.
Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars, mara baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaofanyika June 7, ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.
Meneja wa Timu ya Taifa Stars, Leopold Tasso Mukebezi akiteta jambo na Kepteni wa Timu ya Taifa Stars, Juma Kaseja, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ikulu, walipokutana na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), alipokutana nao, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars Ikulu jijini Dar es Salaam leo alipokutana nao kuwatakia heri ya mchezo wa marudiano na Morocco, nchini humo Juni 7, mwaka huu.

Na Veronica Kazimoto
–MAELEZO, Dar es Salaam
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa, Taifa Stars, kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco
ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la
Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2014.
Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa
ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa
waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa
kupata ushindi wa bao 2-0.
“Maadamu mara ya kwanza mliwashinda
Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi
sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,” amesema Rais Kikwete.
Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya
Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni
mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na kuwataka
wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu
yao ya Taifa.
Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Fenera Mukangara amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali wa michezo nchini ili kuondoa changamoto zinazoikabili
timu hiyo.
Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete
kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo
ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa
timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye
mazoezi na hatimaye kuibuka washindi kwenye mechi
zijazo.
Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi
C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment