TANGAZO


Saturday, May 18, 2013

Mahafali ya 26 ya Ualimu Chuo Al Haramain Islamic

Baadhi ya wahitimu wa Ualimu wa Chuo cha Al Haramain Islamic, wakiwa kwenye mahafali yao ya 26 ya chuo hicho, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk wa bayana.blogspot)

Baadhi ya wahitimu wa kike wa Ualimu wa Chuo cha Al Haramain Islamic, wakiwa kwenye mahafali yao ya 26 ya chuo hicho, Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wazazi na jamaa wa wahitimu wa Ualimu wa Chuo cha Al Haramain wakiwa katika mahafali hayo ya 26, jijini Dar es Salaam leo chuoni hapo.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Nuhu Jabir (kulia), akiwa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Al Haramain, Urassa Suleiman (katikati) na Mkurugenzi wa Elimu wa Bakwata, Rajab Mruma.
Mhitimu Yahya Shaaban Mwinyi akisoma Quran Tukufu kwenye mahafali hayo.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al haramain, Ramadhan Kingalu, akizungumza kwenye mahafali hayo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uongozi, Suleima Nassor na Mwalimu Shaaban Rajab.
Mhitimu Khadija Mohamed, akisoma utenzi kwenye mahafali hayo leo.
Tamthilia, Mwalimu Zoba, akiigiza kufundisha wanafunzi kwa kukariri masomo bila kufuata mpangilio wa ufundishaji na bila kuwa na ujuzi wa ufundishaji.
Wanafunzi wa Ualimu wa mwaka wa pili wakisoma mashairi katika mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa kike wa Ualimu wa Chuo cha Al Haramain Islamic, wakiwa kwenye mahafali yao hayo, Dar es Salaam leo.
Wahitimu wa kiume wa Ualimu wa Chuo cha Al Haramain Islamic, wakiwa kwenye mahafali yao ya 26 ya chuo hicho, Dar es Salaam leo.
Khadija Mohamed, akimpatia rafiki yake, Mhitimu wa Ualimu, Fatuma Haji wakati wa mahafali hayo leo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali yao ya 26 ya Chuo hicho jijini leo.
Wahitimu wakiwa na nyuso za furaha wakati wa mahafali yao hayo leo.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Al Haramain, Urassa Suleiman, akizungumza katika mahafali hayo. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al Haramain, Nurdin Mohamed na kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu wa Bakwata, Rajab Mruma.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al Haramain, Nurdin Mohamed, akizungumza katika mahafali hayo. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Al Haramain, Urassa Suleiman na kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu wa Bakwata, Rajab Mruma.
Baadhi ya wazazi na jamaa wa wahitimu wa Ualimu wa Chuo hicho, wakiwa kwenye mahafali hayo leo.

No comments:

Post a Comment