TANGAZO


Monday, May 13, 2013

Chama cha Watabibu wa Dawa Asili, wasisitiza Amani, Kamanda Mpiga ahimiza Elimu ya Huduma kwa Wateja kwa watoa huduma jijini leo


Mwenyekiti  wa Chama cha Watabibu wa Dawa Asilia Tanzania (ATME), Simba Simba akisisitiza utulivu na amani miongoni mwa wananchi, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu  tukio la ulipuaji wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, jijini Arusha. (Picha zote na Idara ya Habari - Maelezo)


Mwenyekiti  wa  Chama cha Watabibu wa Dawa Asilia Tanzania (ATME), Simba Simba akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu  tukio la ulipuaji wa bomu katika kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, jijini Arusha. Kushoto kwake ni Mratibu wa ATME, Boniventura Mwalongo.



Kamishna Msaidizi Mwandamizi na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga, akisisitiza umuhimu wa Elimu ya Huduma kwa mteja kwa watoa huduma za usafiri nchini, alipokutana na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam.



Mwenyekiti  wa Shirika linalojihusisha na utoaji wa Elimu ya Huduma kwa wateja Kwa wasafirishaji  nchini (SEUTA), Hussein Mhita, akizungumza  na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa mafunzo ya huduma kwa mteja. Kushoto kwake ni  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga.


Kamishna Msaidizi Mwandamizi na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga akikabidhi pikipiki kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo ya huduma kwa mteja.


No comments:

Post a Comment