TANGAZO


Sunday, April 14, 2013

Yanga alipoiadhibu JKT Oljoro ya Arusha, Ligi ya Vodacom Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Sahibu Nayopa wa JKT Oljoro, akiupiga mpira kichwa uliompita Didier Kavumbagu wa Yanga, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda mabao 3-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli la kwanza la timu hiyo, lililofungwa na mlinzi Nadir Haroub 'Canavaro' katika mchezo kati ya timu hizo.

Haruna Niyonzima wa Yanga akijaribu kumpiga chenga Hamis Saleh wa JKT Oljoro wakati wa mchezo huo.

Mashabiki wa Yanga, wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na JKT Oljoro ya Arusha katika mchezo wa Ligi ya Vodacom, Uwnaja wa Taifa, Dar es Salaam jana.

Haruna Niyonzima wa Yanga, akiwatoka wachezaji wa JKT Oljoro katika mchezo huo jana.

Nurdin Mohamed wa JKT Oljoro akikimbilia mpira na Didier Kavumbagu wa Yanga.


Hamis Kiiza wa Yanga, akimruka Majaliwa Sadiki wa JKT Oljoro katika mchezo huo, wa Ligi Kuu ya Vodacom.


Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli lao la pili lililofungwa na Simo Msuva (wa tatu kulia) wa timu hiyo.



Hamis Kiiza wa Yanga, akimkwatua Majaliwa Sadiki wa JKT, Oljoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.




Simon Msuva wa Yanga, akimtoka Karage Mgunda wa JKT Oljoro wakati wa mchezo huo.


Simon Msuva wa Yanga, akipiga krosi langoni mwa JKT Oljoro hukua akikimbizwa na Karage Mgunda wa timu hiyo.




Hadi mwisho wa mchezo huo, ubao wa matangazo ulikuwa ukisomeka Yanga 3, JKT Oljoro 0.

Mchezaji wa Yanga Simon Msuva akimkikwatua mmoja wa wachezaji wa JKT, Oljoro, huku mwengine akiwa amedondoka chini.

No comments:

Post a Comment