TANGAZO


Sunday, April 28, 2013

Simba yaipiga Polisi Morogoro mabao 2-1, Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa, akimiliki mpira hukua akiwa sambamba na wachezaji wenzake, nyuma yao wakifuatwa na John Bosco (13) wa Polisi Morogoro, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Katika mchezo huo, Simba imeshinda mabao 2-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Mrisho Ngassa wa Simba, akijitayarisha kumpiga chenga Rogers Gabriel wa Polisi.


Amri Kiemba wa Simba, akimiliki mpira huku akivutwa jezi na Rogers Gabriel wa Polisi.


Chacha Marwa wa Polisi Morogoro, akiwania mpira na Haruna Chanongo (6) wa Simba.


Mrisho Ngassa, akiwatoka wachezaji wa Polisi Morogoro katika mchezo huo.


Wachezaji wa Simba wakionesha mshikamano kabla ya kuanza kipindi cha pili cha mchezo huo.



Huu ni mpira ambao ulikuwa ukivuka mstari wa goli na kuashiria goli la pili la Simba, lililowekwa kiamiani na mshambuliaji Mrisho Ngassa. 


Mrisho Ngassa akishangilia kwa staili yake huku akipongezwa na Felix Sunzu (kushoto) pamoja na Abdalla Seseme.

Haruna Chanongo wa Simba, akiwatoka John Bosco (aliyeanguka) na Abdalla Mfuko wote wa Polisi Morogoro.


Haruna Chanongo wa Simba, akimtoka Abdalla Mfuko wa Polisi Morogoro katika mchezo huo.


Hadi kwenye dakika za 60, ubao wa matokeo tayari ulikuwa ukionesha Simba mabao 2 na Polisi Morogoro bao 1.

Mrisho Ngassa wa Simba, akitafuta mbinu ya kumtoka Admin Bantu wa Polisi Morogoro.


Mrisho Ngassa wa Simba, akitoa pasi kwa Abdalla Seseme ambaye naye anafuatwa na Admin Bantu wa Polisi Morogoro.


Mrisho Ngassa wa Simba, akikimbizana na Admin Bantu wa Polisi Morogoro, kuuwahi mpira uliokuwa mbele yao.


Mrisho Ngassa, akiruka juu kukwepa kwanja la Chacha Marwa wa Polisi Morogoro katika mchezo huo.

Felix Sunzu wa Simba akichuana na Rogers Gabriel wa Polisi Morogoro katika mchezo huo leo, Uwanja wa Taifa.

Filix Sunzu wa Simba akiwa amelala chini wakati akipambana na Chacha Marwa wa Polisi Morogoro, kuwania mpira.

Mashabiki wa Simba wakishangilia timu yao katika mchezo huo.

Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na Polisi Morogoro.

Hali ya uwanja ilivyokuwa leo, watazamaji wakiwa wamejitokeza wachache katika mchezo huo, kama linavyoonekana jukwa kuu, ambalo hukaliwa na mashabiki wa Simba.

No comments:

Post a Comment