TANGAZO


Sunday, April 28, 2013

Mwenyekiti wa CCM Ilala, Asaa Simba azindua daraja lililojengwa na Mbunge Mussa Zungu Shariff Shamba, Ilala Bungoni

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, akiwa na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, Dar es Salaam leo, katika hafla ya uzinduzi wa daraja la muda kwa wakazi wa maeneo ya Shariff Shamba, Bunguruni Malapa na Ilala Bungoni, lililojengwa kwa msaada wa mbunge huyo.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, akikata utepe ili kuzindua daraja la muda lililojengwa kwa msaada wa Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (kushoto kwake), katika mtaro wa Buguruni Malapa, maeneo ya Shariff Shamba, ambalo hutumiwa na wakazi wa maeneo hayo pamoja na wanafunzi wa Shule za Sekondari Msimbazi na Msingi, Dar es Salaam leo.


 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, akikata utepe ili kuzindua daraja hilo muda lililojengwa kwa msaada wa Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (kushoto kwake), katika mtaro wa Buguruni Malapa, maeneo ya Shariff Shamba, Dar es Salaam leo.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, akiwa na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (katikati), Dar es Salaam leo, wakilikagua daraja la muda linalounganisha maeneo ya Buguruni Malapa na Ilala Shariff Shamba litakalotumiwa na wakazi wa maeneo hayo, mara baada ya kulizindua. Daraja hilo, limejengwa kwa msaada wa mbunge huyo. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Shariff Shamba, Upendo Kisangi.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kulizindua daraja hilo leo.


Diwani wa Kata ya Ilala, Edson Fungo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi huo.


Wananchi wa maeneo ya Shariff Shamba, Ilala Bungoni na Buguruni Malapa, wakiwa kwenye daraja hilo, mara baada ya kuzinduliwa na Mwenyekiti huo wa CCM leo.



Diwani wa Kata ya Buguruni, Magina Lufungulo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi huo jijini leo.


Diwani wa Kata ya Buguruni, Magina Lufungulo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla hiyo, jijini leo.


Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza na waandishi wahabari,wakati wa uzinduzi wa daraja la muda alililolijenga kwa ajili ya wakati wa Buguruni Malapa, Shariff Shamba na Ilala Bungoni.


Kikundi cha burudani cha akinamama wa Mivinjeni, Ilala Shariff Shamba, wakitumbuiza kwa wimbo unaoitwa CCM Hongera, wakati Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala, Asaa Simba, alipokuwa akizindua daraja la muda, Dar es Salaam leo, lililojengwa kwenye mtaro wa Buguruni Malapa kwa ajili ya matumizi ya wakazi wa maeneo hayo na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu.

No comments:

Post a Comment