TANGAZO


Monday, February 11, 2013

Voda, Wizara ya Afya, wazindua mtandano wa madaktari na wataalamu wa afya, kuongea bure kwa simu za Voda

Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom, Salum Mwalim, akitoa maelezo kuhusu mtandao wa Madaktari na wataalamu wa afya, unaojulikana kwa jina la Health Network Programme, mpango ulioanzishwa kwa ajili ya kuwarahisishia utendaji wao wa kazi pamoja na kuboresha kiwango cha mawasiliano yao wenyewe. Madaktari na Wataalamu watatakiwa kujisajili baada ya kuweka kadi ya simu kwa kupiga *149*24hash na kisha kupata maelekezo ya namna ya kujisajili. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Mkurugenzi Mwandamizi wa Mipango na Uendeshaji wa taasisi ya Switchboard, Ali Bloch, akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Hoteli ya Kempisky, Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule, akielezea kuhusu huduma hiyo, kabla ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid kuzungumza na kuuzindua rasmi mtandano huo, hotelini hapo leo.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizungumza kabla ya kuuzindua rasmi mtandano huo, wa Madaktari na Wataalamu wa afya, hotelini hapo leo.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule (kulia) na Mkurugenzi Mwandamizi wa Mipango na Uendeshaji wa taasisi ya Switchboard, Ali Bloch (kushoto), wakinyanyua vipeperushi vya mtandano wa Madaktari na Wataalamu wa Afya wa Healthy Network Programme, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akiuzindua mtandao huo, ambao madaktari nchini wataweza kuwasiliana moja kwa moja katika kutoa huduma za afya kwa wagonjwa kupitia mtandao wa Vodacom bila malipo yoyote. Mtandao huo umebuniwa na Vodacom, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Switchboard kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Kampuni za Vodacom, Swtchboard na wa wizara hiyo, mara baada ya kuuzindua mtandao huo, Dar es Salaam leo. 

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kushoto), akipongezana na Mkurugenzi Mwandamizi wa Mipango na Uendeshaji wa taasisi ya Switchboard, Ali Bloch (kulia), mara baada ya kuuzindua mtandao huo. Katikati anayeangalia ni Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule.

No comments:

Post a Comment