TANGAZO


Thursday, February 7, 2013

TAMWA yatoa Ripoti ya Mradi wa Gewe II kuhusu Utafiti wa Awali wa Ukatili wa Jinsia kwa Wilaya 10 nchini


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa  Habari, Wanawake Tanzania (TAMWA),  Valeria Msoka (kushoto), akionesha ripoti ya utafiti ya Mradi wa Gewe II kwa waandishi wa habari  Dar es Salaam leo, kuhusu utafiti wa awali wa ukatili wa  jinsia uliofanywa na Mashirika ya kutetea haki za  Binadamu yakiwemo Chama cha Wanasheria  wanawake (TAWLA), Chama cha Wanasheria  wanawake Zanzibar (ZAFELA), Kituo cha  Usuluhishi (CRC), Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na TAMWA Bara na Zanzibar. Kulia ni Salome Assey kutoka Chama cha Wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi  wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),  Valeria Msoka (kushoto), akizungumza katika  mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,  wakati akitoa taarifa ya Mradi wa Gewe II kuhusu utafiti  wa awali za ukatili wa kijinsia uliofanywa na 
Mashirika ya kutetea haki za Binadamu yakiwemo  Chama cha Wanasheria wanawake (TAWLA), Chama cha Wanasheria wanawake Zanzibar  (ZAFELA),  Kituo cha Usuluhishi (CRC), Mtandao wa Jinsia  Tanzania (TGNP) na TAMWA Bara na Zanzibar. Kulia ni Mratibu wa TAMWA,  Zanzibar  Mzuri Issa na Ofisa Programu wa TGNP, Felister Mwanyingili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi  wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valeria Msoka (katikati), akiwa na viongozi wa Mashirika ya Kutetea haki za Binadamu. Kutoka  kushoto ni Salome Assey kutoka TAWLA, Elizabeth Muhangwa wa Kituo cha  Usuluhishi (CRC) , Fesliter Mwanyingili  kutoka TGNP na  Mratibu wa TAMWA Zanzibar, Mzuri Issa.
Ofisa Programu wa TGNP, Festa Mwanyingili (katikati), 
akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu  ripoti hiyo. Kulia ni Mratibu wa TAMWA Zanzibar,  Mzuri Issa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valeria Msoka
Waandishi wa habari wakipokea taarifa hiyo. 

Mwakilishi kutoka Kituo cha Usuluhishi (CRC), Elizabeth Muhangwa, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.
Viongozi wa Mashirika ya kutetea haki za binadamu wakipitia ripoti hiyo. (Picha zote na Habari namwaibale.blogspot)

Na Dotto Mwaibale

Utafiti uliofanywa na mashirika ya kutetea haki za binadamu 
katika utafiti wa awali kuptia mradi wa Gewe II kuhusu 
ukatili wa kijinsia hapa nchini umebaini waathirika wa 
matukio hayo hawana sehemu maalum ya kupeleka 
malalamiko yao.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo Mkurugenzi 
Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake 
Tanzania (TAMWA),
Valeria Msoka, wakati akizungumza na waandishi wa 
habari wakati akitoa taarifa ya utafiti wa awali za
 ukatili wa kijinsia.

Alisema utafiti huo umefanywa na Mashirika matano 
ya kutetea haki za Binadamu ambayo ni Chama cha 
Wanasheria wanawake (TAWLA), Chama cha 
Wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA),
 Kituo cha Usuluhishi (CRC), Mtandao wa Jinsia 
Tanzania (TGNP) na Chama cha waandishi 
Habari wanawake Tanzania (TAMWA) 
Bara na Zanzibar.

Alisema utafiti huo umeonesha asiliamia 17 ya wananchi wanauelewa wa sheria za ukatili hali imayopelekea 
kutokufuatilia haki zao wakati wa uvunjaji na 
wakati mwingine kutoripoti kabisa kesi hizo.

Alizitaja wilaya zilizofanyiwa utafiti ghuo kuwa ni 
Wete (Pemba kaskazini), Magharibi Unguja, Kusini 
Unguja (Kusini Unguja), Kisarawe (Pwani), 
Newala (Mtwara), Lindi Vijijini (Lindi), Mvimero
(Morogoro) na wilaya mbili za Kinondoni na Ilala
 (Dar es Salaam).

Msoka aliitaja Lindi Vijijini kuwa ndio wilaya 
inayoongoza 
kuwa na uelewa mdogo wa asilimia 12 ambapo 
asilimia 21 ya uelewa kwa Wete Zanzibar kuwa 
 ni mkubwa kuliko wilaya zote ulipofanyika utafiti huo.

"Ofisa mmoja wa Polisi Lindi alisema kesi  nyingi 
huripotiwa katika hatua ya familia na hufikishwa 
mahakamani baada ya kushindwa kupata suluhu hivyo 
kuwa katika hatari ya kupata haki" alisema Msoka.

Aliongeza kuwa utafiti huo kwa ujumla uliona 
asilimia 47 za kesi huripotiwa katika Serikali za vijiji,
asilimia 25 huripotiwa polisi nyingine huripotiwa 
Kamisheni ya Haki zaaa Binadamu, Mashirika 
ya Hakli za Binadamu na kwa wanasheria 
wanaongoza (Para Legals).

"Hali hiyo ya kutokuwa na mfumo maalum wa kuripoti 
inaweka mazingira ya kutopatika kwa haki na pia 
kukosekana kwa takwimu sahihi ya kesi za ukatili"
 alisema Msoka.

Alisema taarifa hiyo inaonesha kuwa wananchi 
hawana majukwa ya kukaa pamoja na kujadili 
changamoto zao am,bapo ni asilimia 13.5 ndiyo 
wanachama wa vyama vya kijamii 
(Civil Society Associations).

Msoka alisema kwa pamoja Mashirika hayo yatekeleza mpango wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (GEWE) ambao unafanywa kwa mashirikiano na Serikali ya Denmark.

No comments:

Post a Comment