TANGAZO


Saturday, February 9, 2013

Mofisa Habari wa Serikali wamaliza kikao chao mjini Dodoma, watembelea Bunge na kushiriki upandaji miti UDOM

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo), Raphael Hokororo, akiwafundisha Maofisa Habari na Mawasiliano  wa Serikali kutoka Wizara, Taasisi, Wakala, Mashirika ya Umma, Mikoa na Wilaya, upigaji wa picha bora  za mnato kwa  matumizi ya habari, wakati wa kuhitimisha kikao cha maofisa hao, mjini Dodoma jana. 

Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodoma juzi, kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara. 

Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodoma kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana, ambaye alikua miongoni mwa waalikwa waliohudhuria Kikao kazi cha Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, akiongea na mafiasa hao, mjini Dodoma jana. 

Baadhi ya viongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi wa Idara hiyo, Assah Mwambene (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Usajili wa Magazeti, Raphael Hokororo (wa pili kushoto), wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kuwasalimia waheshimiwa Wabunge mara baada ya kuombwa na Spika Makinda, wakiwaongoza Maofisa Habari wa Serikali. 

Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, wakiwasili Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana, kushiriki zoezi la upandaji wa miti chuoni hapo, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuhifadhi mazingira ya chuo hicho. 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga akizindua zoezi la upandaji wa miti lililowahusisha Maofisa Habari wa Serikali katika Kampasi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), jana. 

Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, wakiendelea na zoezi hilo, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana. 

Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma. 

Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, wakiendelea na zoezi la kwenda kupanda miti, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana. 


Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Swalehe Chondoma, akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana. (Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO)

No comments:

Post a Comment