TANGAZO


Saturday, February 9, 2013

Mama Tunu Pinda ahudhuria Ufungwaji Kikao cha Bunge, mjini Dodoma

Mbunge Mussa Azzan 'Zungu' wa Ilala, Dar es Salaam na Waziri Mkuu mstaafu, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Edward Lowassa (kulia), wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma mara baada ya kikao cha Bunge kufungwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana.

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati), akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kulia), nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana wakati kikao cha Bunge kilipofungwa jana. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati, mara baada ya kulifunga rasmi Bunge, mjini Dodoma jana. 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati, mara baada ya kulifunga rasmi Bunge, mjini Dodoma jana. (Picha zote na Chris Mfinanga)

No comments:

Post a Comment