TANGAZO


Sunday, February 17, 2013

Kombe la Ligi ya Mabingwa, Simba yakubali kichapo mbele ya Libolo FC ya Angola, Uwanja wa Taifa

Haruna Chanongo wa Simba (kulia), akiwania mpira na Carlos Almeid wa Libolo ya Angola, wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Libolo ilishinda mchezo huo kwa bao 1-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
 
 
Haruna Chanongo wa Simba (kulia), akiwania mpira na Carlos Almeid wa Libolo ya Angola, wakati wa mchezo huo.

Golikipa wa timu ya Libolo ya Angola, Landu Mavanga, akishangilia bao pekee la timu hiyo, katika mchezo huo, dhidi ya Simba.


Golikipa wa timu ya Libolo ya Angola, Landu Mavanga akishangilia kwa kusujudu, bao pekee la timu hiyo, katika mchezo huo, dhidi ya Simba.

 Amri Kiemba wa Simba, akimtoka Pedro Libero wa Libolo FC ya Angola.

Antonio Kasule wa Libolo FC, akiuwahi kwa kuruka juu, mpira uliokuwa ukidhibitiwa na Haruna Moshi.
 
 Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo dhidi ya Libolo FC ya Angola.

Golikipa wa timu ya Libolo ya Angola, Landu Mavanga, akiudaka mpira wa kona uliokuwa umeelekezwa langoni kwake, huku Amri Kiembe wa Simba, akijitahidi kuufikia kwa ajili ya kuupiga kichwa mpira huo.

 Nassoro Said 'Cholo' wa Simba, akikimbilia mpira sambamba na Dario Cardoso wa Libolo FC.

 Ubao wa matokeo ukionesha Simba 0 na Libolo ya Angola bao 1.

 Haruna Chanongo wa Simba, akimtoka Dario Cardoso wa

timu ya Libolo FC ya Angola.
 
Haruna Chanongo wa Simba, akipambana na Dario Cardoso

wa timu ya Libolo FC ya Angola.

 JUma Nyoso wa Simba akimtoka Pedro Libero wa Libolo FC ya Angola.

 Haruna Moshi akipiga krosi mbele ya Sidnei Mariano wa FC Libolo.

 Mrisho Ngassa wa Simba akimtoka Dario Cardoso wa Libolo FC katika mchezo huo.

 Mashabiki wa Yanga wakiikejeli Simba baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Libolo FC ya Angola.

 Shomari Kapombe akitafuta mbinu ya kumtoka Pedro Libero wa Libolo FC ya Angola.

Haruna Chanongo wa Simba, akiwatoka Gamawel Musumari (kulia) na Dario Cardoso (katikati) wa timu ya Libolo FC ya Angola.

Mashabiki wa Yanga wakiipa sapoti timu ya Libolo FC ya Angola.

No comments:

Post a Comment