
Golikipa wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, Posnett Omony,
akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry
Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54. Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele
mpaka dakika 90 kwa kuinyuka goli 2-1, timu ya Black Leopards, kwenye mchezo wao wa
marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba, jijini
Mwanza jana. (Picha zote kwa hisani ya Ahmed Michuzi)

Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili,
lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili, mnamo dakika ya 54 kwa njia ya
penati.

Mchezaji wa wa timu ya Yanga, David Luhende akitaka
kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards, Moses Kwena, kwenye mchezo wao wa
marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza jioni ya
jana.

Pichani, Golikipa wa Black Leopards, Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na
mchezaji wa Yanga, Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya
saba.

Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga, akifanya jitihada za
kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards, Victor Kamhuka.

Mchezaji wa wa timu ya Yanga,
David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards, Moses
Kwena, kwenye mchezo wao, wa marudio uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.

Baadhi ya mashabiki wa Mpira wa Miguu, wakiwa wamepanga mstari
kwa ajili ya kununu tiketi za kujionea kandanda, safi kabisa kati ya timu ya
Yanga na Black Leopards ya Afrika kusini.

Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya
pamoja.

Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo
huo, ambapo timu ya Yanga, imetoka kifua mbele kwa kushinda goli 2-1, dhidi ya timu ya Black
Leopards ya Afrika Kusini, katika mchezo uliochezwa jana, uwanja wa CCM-Kirumba
jijini Mwanza.

Wachezaji wa timu ya Yanga na Afrika Kusini wakisalimiana kabla ya mtanange kati ya timu hizo kuanza.

Kikosi cha timu ya Black
Leopards.

Benchi la ufundi la timu ya
Yanga

Ilikuwa ni patashika ngua kuchanika,mchezaji wa timu
ya Yanga,Jerry Tegete akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry
alifanikiwa kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha
pili.

Nginja nginja
tuu

Makocha wakipongezana mara baada ya mpira
kuisha.

Sehemu ya Umati wa mashabiki wa timu ya
Yanga, wakiangalia mchezo huo jana.

Mashabiki wakiwa kwenye
mstari kwa ajili ya kuingia uwanjani.

Mashabiki wa timu ya Yanga, wakiwa wamejazana Uwaja wa CCM Kirumba, kushuhudia mpambano huo.


No comments:
Post a Comment