![]() |
| Waziri wa Elimu wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna |
JUMLA wanafunzi 11,195, wamechaguliwa kujiungia Kidatu cha Tatu kwa mwaka wa masomo 2013 katika Skuli mbalimbali za Unguja na Pemba ambapo kati yao wasichana ni 6,768 na wavulana ni 4,427.
Aidha
Wanafunzi 17,511 wamefaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka huu ambapo kati yao,
Wasichana ni 9,652 na Wavulana 7,859 .
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna amebainisha hayo leo wakati alipokuwa akitoa tathimini ya matokeo ya mitihani hiyo huko ofisini kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Amesema kuwa Wanafunzi waliofanya mtihani
wa kuingilia Kidato cha Tatu walikuwa 19,679 ambapo kati yao Wasichana walikuwa
11,045 na wavulana 8644 sawa na asilimia 93.6 %.
Aidha
ameongeza kuwa ufaulu wa kidato cha Tatu umeongezeka kwa asilimia 0.8
ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Kwa
upande wa Mtihani wa Darasa la Saba Waziri Shamhuna amesema jumla ya Wanafunzi
waliofanya mtihani huo walikuwa 23,039 kati yao wasichana walikuwa 12,236 na
wavulana 10,803.
Akielezea Skuli zilizoshika nafasi ya juu
kwa matokeo ya Darasa la Saba Waziri Shamhuna amesema ni pamoja na Kizimbani
iliyopo Wilaya ya Wete Pemba na Skuli za Wazazi na Mkunazini zote za Wilaya ya
Mjini Unguja.
Aidha
amezitaja Skuli zilizofanya vibaya matokeo ya Darasa la Saba kuwa ni Kojani,
Ukunjwi na Makoongwe zote za Kisiwani Pemba.
Kwa upande wa Matokeo ya Kidato cha Pili skuli zilizofanya vyema kuliko nyingine ni Mtoni iliyopo Wilaya ya Magharibi Unguja na Skuli za Msuka na Kiuyu zote za Wilaya ya Micheweni Pemba.
Akielezea Skuli zilizofanya vibaya mtihani
wa Kidato cha Pili Waziri Shamhuna amesema ni Skuli za Mwenge iliyopo Wilaya ya
Magharibi na Skuli za Mfuru matonga na Kinyasini zote za Kaskazini A
Unguja.
Waziri Shamhuna amezitaja pia Skuli ambazo
zitalazimika kufungwa kutokana na kupasisha idadi ndogo ya Wanafunzi ambazo ni
Bwefum, Umbuji, Uzi, Ubago,Pongwe Pwani, Michanvi,Mtende,Kisiwa Panza,Makongwe
na Ndagoni.
Ameongeza kuwa jumla ya Kesi za udanganyifu
12 ziliripotiwa kwa wanafunzi wa Kidato cha pili ambapo Wizara imeamua kwafutia
matokeo wanafunzi waliohusika na Udanganyifu huo.


No comments:
Post a Comment