TANGAZO


Wednesday, January 9, 2013

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa na Bibi Shamba


Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akipata maelezo kuhusu aina ya mbegu ya mahindi, iliyotumika kutoka kwa Grace Hokororo, ambaye ni Bibi Shamba wa Kata ya Itenka, wakati alipokuwa akikagua shamba darasa analolisimamia kwenye kijiji cha Itenka, wilayani Mlele, mkoani Katavi, juzi, Januari 6, 2013. Waziri Mkuu, alifurahia kazi yake na kuahidi kumpatia pikipiki imsaidie kutembelea vijijiji vingine, vinne anavyovisimamia. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Bibi Shamba wa Kata ya Itenka, Grace Hokororo, akimshukuru Waziri Mkuu Mizengo kwa kufanya ukaguzi kwenye shamba darasa analolisimamia katika Kijiji cha Itenka, wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi. Aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie kutembelea vijijiji vingine, vinne anavyovisimamia.

Bibi Shamba wa Kata ya Itenka, Grace Hokororo, akipokea zawadi ya sh. 305,000,  kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambazo zilichangwa papo hapo na watu alioandamana nao, ili kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye shamba darasa. Wa pili kulia ni Joseph Laurent, anayesimamiwa na bibi shamba huyo, ambaye shamba lake lilikaguliwa na Waziri Mkuu katika kijiji cha Itenka, wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi. Pia aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie kutembelea vijijiji vingine, vinne anavyovisimamia.

No comments:

Post a Comment