TANGAZO


Sunday, January 13, 2013

Wanataaluma, Taasisi za Elimu, Wanafunzi Elimu ya Juu, watoa maoni ya Katiba MpyaMjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Awadh Said (kulia) akiongea na viongozi wa Jukwaa la Mamlaka na Taasisi zinazosimamia na kuthibiti ubora wa elimu nchini ulioongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Sifuni Mchome (mwenye tai katikati). Jukwaa hilo lilikutana na Tume katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumapili, Jan 13, 2013) kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya. 

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Awadh Said (kulia), akiongea na viongozi wa Jukwaa la Mamlaka na Taasisi zinazosimamia na kudhibiti Ubora wa Elimu nchini, ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Profesa Sifuni Mchome (mwenye tai katikati). Jukwaa hilo lilikutana na Tume katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo, Jumapili, Januari 13, 2013 na kuwasilisha maoni yake, kuhusu Katiba Mpya. (Picha zote na Tume ya Katiba)
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Humphrey Polepole (kulia), akiongea na viongozi wa Jukwaa la Mamlaka na Taasisi zinazosimamia na kudhibiti Ubora wa Elimu nchini ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Profesa Sifuni Mchome (kushoto). Jukwaa hilo lilikutana na Tume katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo, Jumapili, Januari 13, 2013 na kuwasilisha maoni yake, kuhusu Katiba Mpya.
Mjumbe wa Jukwaa la Mamlaka na Taasisi zinazosimamia na kudhibiti Ubora wa Elimu nchini, Dk. Primus Nkwera ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE), akitoa maoni ya jukwaa hilo, kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo, Jumapili, Jan. 13, 2013. Kulia ni Mjumbe wa Tume, Humphrey Polepole na kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Profesa Sifuni Mchome.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Mamlaka na Taasisi zinazosimamia na kudhibiti Ubora wa Elimu nchini, Profesa Sifuni Mchome, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), akitoa maoni ya jukwaa hilo, kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, uliofanyika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo, Jumapili, Jan. 13, 2013. Kulia ni Wajumbe wa Tume, Awadh Said na Humphrey Polepole.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Mamlaka na Taasisi zinazosimamia na kudhibiti Ubora wa Elimu nchini, Profesa Sifuni Mchome, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), akitoa maoni ya jukwaa hilo, kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, uliofanyika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo, Jumapili, Jan. 13, 2013. Kulia ni Wajumbe wa Tume, Awadh Said na Humphrey Polepole.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Nchini (TAHLISO), mara baada ya viongozi hao, kuwasilisha maoni ya umoja huo, kuhusu Katiba Mpya kwa Tume, Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo, Jumapili, Jan. 13, 2013.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), Dk. Francis Michael (kushoto) akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, uliofanyika katika Ofisi za Tume jijini, Dar es Salaam leo, Jumapili, Jan. 13, 2013. Wengine ni Dk. Agnes Mwasumbi kutoka Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARISA) na Edson Baradyana kutoka Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), Dk. Francis Michael, akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, uliofanyika katika Ofisi za Tume jijini, Dar es Salaam leo, Jumapili, Jan. 13, 2013. Wengine ni Dkt. Felician Komu (kushoto) kutoka Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARISA) na Bw. Edson Baradyana (kulia) kutoka Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA).

No comments:

Post a Comment