TANGAZO


Sunday, January 13, 2013

Wanane wauwawa Somalia kwenye operesheni


Wakaazi wa mji mmoja wa kusini mwa Somalia wanasema raia wanane waliuwawa katika jaribio lilofanywa na makamando wa Ufaransa kumkomboa mwananchi mwenzao aliyezuwiliwa na wapiganaji.
Ramani ya mji wa Bulo Marer
Walioshuhudia tukio hilo wanasema watu wane walikufa wakati makamando wa Ufaransa walipotua nje ya mji wa Bulo Marer.
Wengine walikufa katika mapambano ya risasi.
Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa alikufa Jumamosi kwenye operesheni hiyo na mwengine ametoweka.
Wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab ambao walikuwa wanamzuwia askari wa ujasusi wa Ufaransa walisema afisa huyo yuhai, lakini Ufaransa inasema pengine aliuwawa.

No comments:

Post a Comment