Wanajeshi wa Mali
Majeshi ya Mali, yameutwaa mji muhimu wa Douentza, ulio
katikati ya nchi hiyo, kutoka kwa wapiganaji wa Kiislam.
Habari zimesema, jeshi la Mali pia limeanzisha operesheni ya kijeshi
kuurejesha mji wa Konna.
Amesema mgogoro wa Mali, ni mgogoro wa dunia ambao NATO inatakiwa kuingilia kati kama ilivyofanya nchini Afghanistan kukabiliana na vikundi vya Taleban na al-Qaeda.
Mwanajeshi wa Mali akiwasaka wapiganaji wa
waasi
Baadhi ya viongozi wa Ulaya wameelezea wasiwasi kwamba wapiganaji wa kiislam kutoka maeneo mengine duniani, wanaweza kutumia eneo kubwa la Mali, linalodhibitiwa na wapiganaji wa Kiislam, ambalo sawa na ukubwa wa Ufaransa, kufanya mashambulio dhidi ya nchi za Ulaya.
Mwezi uliopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, liliidhinisha mipango ya kupeleka askari 3,000 kutoka nchi za Afrika Magharibi, kupigana dhidi ya wapiganaji wa Kiislma nchini Mali.
Lakini maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema hawakutarajia upelekaji wa askari hadi mwezi Septemba 2013.
Mapigano makali
Wapiganaji wa waasi wa Mali
Mujao wamekuwa wakiudhibiti mji wa Douentza tangu Septemba 2012.
Taarifa zinasema jeshi pia limeanzisha operesheni ya kijeshi kuwaondoa wapiganaji wa Kiislam kutoka mji wa Konna, ambao uko pembezoni mwa eneo linalodhibitiwa na serikali na mji mkuu wa jimbo wa Mopti.

No comments:
Post a Comment