TANGAZO


Sunday, January 6, 2013

Vodacom yatembelea na kusaidia Sober House Pemba




Na Martin Kabemba, Zanzibar

Kampuni ya simu ya Vodacom Foundation imekabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vikiwemo mchele, mafuta ya kupikia, sabuni na vifaa vingine kwa ajili ya vijana wanaolelewa kutokana na utumiaji madawa ya kulevya kwenye nyumba ya Sober House ya wanawake, iliyoko  Mombasa mjini Zanzibar jana.

Kampuni hiyo, imetenga jumla ya Sh. milioni 50 kwa ya matumizi ya kuhudumia vijana hao nchini Tanzania.


Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon (kushoto), akikabidhi msaada huo kwa Msimamizi wa makazi ya vijana walioathirika na madawa ya kulevya (Sober House) ya wanawake Unguja, Fatuma Sukwa jana.
Msimamizi wa makazi ya vijana hao (Sober House) ya wanawake Unguja, ambaye pia ni Msaidizi Katibu wa taasisi ya Zanzibar Bila Madawa 'Zanzibar Free Drugs', Bi. Fatuma Sukwa, akitoa shukrani baada ya kukabidhiwa msaada huo toka kwa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Foundation jana.
Baadhi ya Vijana wa Sober House, Unguja, wakisikiliza maelezo wakati wa makabidhiano ya msaada wa vyakula kutoka Kampuni ya Vodacom Com kupitia kitengo chake cha misaada kwa jamii cha Vodacom Foundation jana. (Picha zote na Martin Kabemba)

VODACOM YASADIA VIJANA PEMBA

Meneja wa Kituo cha Kutibu Kuachana na Matumizi ya Dawa za Kulevya (Sober House) cha Chake-chake, kisiwani Pemba, Mohammed Kassim akisoma maelezo ya matumizi ya dawa ya kusafisha choo mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), kwa niaba ya Taasisi ya Vodacaom Foundation katika hafla iliyofanyika kituoni hapo, mwishoni mwa wiki. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon (wa pili kushoto). Vodacom Foundation imevipatia vituo vinne vya aina hiyo vya Wete na Chake-chake, vyakula na vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya programu ya pamoja na Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi moja ya ndoo ya mafuta kwa Mratibu wa Vituo vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo (Sober House), za Wete kisiwani Pemba, Abdulwaheed Said kwa niaba ya Vodacom Foundation. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom, Salum Mwalim (wa kwanza kushoto). Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki, Chakechake Pemba.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi kiroba cha mchele kwa Meneja wa Kituo cha Kusaidia Watumiaji wa Dawa za Kulevya Kuachana na Matumizi ya Dawa hizo (Sober House) cha Chakechake, Pemba, Abdulwaheed Said kwa niaba ya Vodacom Foundation. Wanaoshuhudia ni Menejja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom, Salum Mwalim (wa kwanza kushoto). Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kituoni hapo.
Mratibu wa Vituo vya Kutibu Watumiaji wa Dawa za Kulevya Kuacha Kutumia Dawa hizo (Sober House) za Wete Pemba, Abdulwaheed Said akishukuru kwa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kutoka Vodacom Foundation vilivyotolewa kwa Sober House nne za kisiwani Pemba. Kutoka Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, Meneja wa Sober Hosue ya Chake-Chake, Mohammed Kassim na Meneja wa Mahusiano ya Nje Salum Mwalim. Mkabidhiano hayo yamefanyika mishoni mwa wiki mjini Chakechake.

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom mwishoni mwa wiki imetembea vituo vya kusaidia watumiaji wa dawa kulevya kuachana na dawa hizo – Sober House Kisiwani Pemba ziara iliyomjumuisha Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa.

Ziara hiyo ililenga kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo vyakula na vitu vingine vya matumizi ya ndani ikwemo dawa za kusafishia vyoo, sabuni katika kwa Sober House nne zilizopo Chakechake na Wete.

Akizungumza katika Sober House ya Chakechake Waziri Profesa Mbarawa aliwataka wateja wa vituo hivyo ambao wengi wao ni vijana kuhakikisha matumaini waliyoyaonyesha ya kutaka kuachana na matumzi ya dawa za kulevya hayapotei.

Waziri Prof Mbarawa amesema uamuzi waliouchukua wa kutaka kuachana na matumiz ya dawa za kulevya ni wa msingi na unawawezesha kurudi katika maisha yao ya kawaida sanjari na kutimiza ndoto za maisha walizokuwa nazo hapo kabla ya kujitumbukiza katika matumizi ya adwa za kuelvya na kuwapotezea dira ya maisha.

“Nimejulishwa kwamba kuingia katika nyumba hii ni lazima mtumiaji mwenyewe ukubali kuwa yupo tayari kuachana na dawa kulevya hilo ni jambo jema na linalonyesha kwamba mnayo matumaini ya kurudi katika maisha ya kawaida yasiyohusisha matumizi ya dawa za kulevya na aina nyengine ya vilevi.”Alisema Prof. Mbarawa

“Mnayo mifano ya mafanikio ya wale ambao wameshapitia program hizi na wamefanikiwa na hata nyie hapa mpo ambao tayari mna siku nyingi za usafi bila kutumia dawa ama kilevi cha aina yoyote hivyo ni rai yangu kwenu kuendelea kuamini katika matumaini mliyo nayo.”Aliongeza Profesa Mbarawa.

Akizungumzia juhudi za serikali katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya nchini Waziri huyo amesema serikali imekuwa ikifanya kila juhudi katika kukomesha biashara hiyo.

“Serikali na hata Rais Kikwete(Jakaya)binafsi amekuwa akifanya juhudi kubwa katika kukomesha biashara hii na amekuwa akitukalisha chini mawaziri na kutuelezea mikakati mbalimbali ikiwemo kutuonesha mikanda ya video inayoonyesha athari za dawa za kulevya ambazo zinasikitisha mno.”Alisema Waziri Prof Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema changamoto kubwa inayokabili vita hii ni namna ya kukamalisha udhibiti dhidi ya mhalifu au washukiwa wanaojihusisha na biashara hizi haramu ili kuwafikisha mahakamani na hatimae sheria kuchukua mkondo wake lakini hata hivyo juhudi zipo na kuwaomba wateja hao wanaopata nafuu kutoa ushirikiano huku akkiwapongeza Vodacom.

“Nawapongeza sana Vodacom kwa kufika hapa na kuwasaidia vijana hawa ambao bado wanaweza kuwa na mchango mkubwa kwa taifa.Mimi ni mara yangu ya kwanza kutembelea Sober House, nimeguswa na naahidi kuwaleta wadau zaidi kusaidia nyumba hizi ili kazi inayofanyika humu iimarike na kutoa mchango zaidi katika mapambanao dhidi ya dawa za kuelvya nchi.”Alisema Prof. Mbarawa
Awali Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon alisema Vodacom imefika katika nyumba hizo ikitekeleza kwa vitendo dira yake ya kusaidia makundi yenye uhitiji kupitia program ya Pamoja na Vodacom inayotekelezwa kwa michango ya wafanyakazi na kampuni.

“Hatukifika hapa kwa bahati mbaya tunajua kazi kubwa inayofanyika katika nyumba hizi na kwa makusudi tumezijumiisha katika makundi yakunufaika na program yetu ya Pamoja na Vodacom ili kuunga mkono kazi hiyo na kuonesha upendo wetu kwenu.”

“Tatizo la dawa za kulevya sio la mtu mmoja linatugusa sote kama sio ndani ya familia basi kuna ndugu, jirani au hata rafiki.”Alisema Lyon na kuongeza “Wito wangu mkubwa ni kuwaomba kujitahidi kuhakikisha hamrudii kutumia dawa za kulevya na aina nyengine za vilevi mara mnapokamilisha matibabu yenu na kurudi uraiani.”

Kwa upande wake Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom amepongeza utayari wa wale ambao walikuwa watumiaji kabla ya kuacha na kuona umuhimu wa kusaidia wenzao ili nao waache na kurudi katika maisha mema na masafi.
“Waanzilishi wa nyumba hizi(Sober House) ni watu wenye ujasiri na upendo mkubwa katika jamii wameliona tatizo na wamekuwa tayari kutoa ujuzi, nguvu, mali na muda wao kusaidia wengine, naamini hii ni silaha moja muhimu katika mapambano dhidi ya dawa kulevya nchini.”Alisema Mwalim.

Wakizungumza kupitia risala yao iliyosomwa kwa niaba yao na Abdala Hassan watu hao walio katika tiba maarufu wateja wanaopata nafuu wamesema haikuwa rahisi kwao awali kuamini kuwa wangeweza kubadilika na kurudi katika maisha ya kawaida ya kutotumia dawa za kulevya.
“Na sisi tulio mele yenu ni wateja tunaopata nafuu kwa hiari zetu bila ya kulazimishwa na mtu yeyote tumeamua kubadilika kutoka janga la dawa za kulevya baada ya kuchoshwa na hali za kudhalilika,kupoteza utu wetu, kutoheshimiwa, kuwa mzigo katika familia na jamii.”Alisema Hassan.

“Ni kweli tulikuwa hatuna maadili mema kila mmoja ana historia yake ya nyuma. Tuna shukrani kubwa kwa waasisi wa umoja huu wa N.A (Narcotics Anonymous) na Sober House kwa sababu sasa tunaishi kwa amani, upendo, utulivu bila kufanya uhalifu wa aina yoyote na tunamatumaini na matarijio ya kurejea kuwa wazalishaji bora katika jamii.”Aliongeza Hassan.

Katika kisiwa cha Pemba zipo jumla ya Sober House tano zilizo chini ya uongozi na usimamizi wa watu binafsi ambazo Vodacom Foundation ilizipatia chakula na mahitaji mengine.Hata hivyo warataibu wa Sober House wameiomba seriklai kuzitupia macho na kuziwezesha.

Vodacom Foundation iliandaa pia chakula cha mchana kwa ajili ya wateja wanaoptaa nafuu walio katika vituo hivyo mlo ambao ulimhusisha pia waziri Profesa Mbarawa na wafanyakazi wa Vodacom waliotembelea.

No comments:

Post a Comment