TANGAZO


Thursday, January 10, 2013

Msanii Wema Sepetu na wenzake wanogesha uzinduzi wa kampeni ya Kilimo Kwanza Kata ya Kwadelo, Kondoa


 Diwani Omary Kariati wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, baada ya kuwashili katika kata hiyo jana kuzindua Kampeni ya Kilimokwanza kwa Vijana wa Kata hiyo. Kutokana na juhudi za diwani huyo hivi sasa kata hiyo inayo matrekta 60 yanayotumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya alizeti na ufuta.
 Wasanii wa filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B',  Vicent Kigosi 'Ray', Irene Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rick Rich' walipowasili Kwadelo kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya Kilimo Kwanza kwa vijana wa Kata hiyo.
Wazee wa Kwadelo wakati wakimsubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao.
 Baadhi ya kinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo.
 Ray akipozi picha na wazee wa Kwadelo.
Kariati akiwa na wasanii hao kwenye trekta kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo.
Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Diwani wa  Kata ya Kwadelo, Kondoa, Omary Kariati.
 Msanii Irine Uwoya naye akilijaribu trekta kwenye uzinduzi huo.
KWADELO HOYEEEEEE! J B akihamasisha wakati wakiwa kwenye trekta la Kilimo Kwanza, wakati wa uzinduzi huo.
 Treka likionyesha mfano wa ulimaji wa kisasa kwenye shamba la Shule ya Sekondari ya Kwadelo, wakati wa uzinduzi huo.
 KITUKO: Panzi! Panzi! Panzi!, Wema Sepetu (shati ya kijani), akifunika uso wake kwa kipochi chake, huku akipiga kelele na kujiingiza katika kundi la wazee,  kwa sababu ya kuogopa panzi aliyemdandia wakati wa shughuli za uzinduzi huo shambani hapo.
Wasanii JB na Wema wakila mapozi shambani, wakati wakienda sehemu ya uzinduzi huo.
 Wema akitangaza kuzindua kampeni hiyo.
Wasanii Wema na JB, wakishuhudiwa na Ray na Diwani Omari Kariakti (wa pili kushoto), wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo, walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani huyo, fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe ambaye ni Mzee wa heshima wa kata hiyo.
Diwani Kariati akikagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika moja ya vijiji vya Kata ya Kwadelo, kufuatia mvua zoinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
Diwani wa Kwadelo, Omar Kariati, akioneshwa maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko.
Wazee wakiomba dua ya kheri baada ya shuguli za uzindizi wa Kampeni ya Kilimo Kwanza kwenye Kata hiyo na kukagua maeneo ya walioathiriwa na mafuriko. (Picha zote kwa hisani ya Bashir Nkoromo wa Daily Nkoromo Blog)

No comments:

Post a Comment