TANGAZO


Tuesday, January 29, 2013

Mnada wa ndege ya Rais Malawi

 


Rais Joyce Banda amekataa kuitumia ndege hiyo kwa usafiri wake
 

Serikali ya Malawi imewaalika watu wenye nia ya kununua ndege ya rais wa nchi hiyo yenye viti 14.
Ndege hiyo inauzwa kama hatua ya rais kupunguza matumizi ya pesa za serikali.

 
Duru katika ofisi ya rais Joyce Banda, zinasema kuwa ndege hiyo itauzwa kwa yule atakayeinunua kwa bei ya juu zaidi.

Mtangulizi wake, hayati Rais Bingu wa Mutharika, alikashifiwa vikali kwa kununua ndege hiyo miaka mitano iliyopita kwa takriban dola milioni 8.9.

Wahisani walisitisha msaada wa dola milioni nne nukta nne kwa Malawi punde baada ya serikali ya Mutharika kuinunua ndege hiyo.

Bi Banda amekataa kusafiri kwa ndege hiyo, tangu kuchukua hatamu za uongozi mwezi Aprili mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla cha Mutharika.

'Nafuu kutumia'

Alisema kuwa pesa zitakazopatikana baada ya kuiza ndege hiyo kuuzwa , zitatumiwa kutoa huduma muhimu kwa watu maskini wa Malawi.

Duru zilisema kuwa ndege hiyo iko katika hali nzuri kuweza kutumiwa, na inaweza kupaa kwa kilomita 8,380 bila kusimama.

Mnada utakuwa wazi kwa yeyote atayetaka kuinunua

Wakati Mutharika alipoinunua ndege hiyo, alisema haitaigharimu serikali pesa nyingi kuitumia.
Ingawa baadaye upinzani pamoja na wahisani walimtuhumu kwa kutumia vibaya pesa za serikali.
Malawi ni mojawapo ya nchi maskini sana barani Afrika.

Ilikumbwa na maandamano juu ya kupanda kwa bei ya maisha rais Mutharika alipokuwa anakamilisha muhula wake wa utawala.

Tangu kuitawala nchi hiyo, Bi Banda amechukua hatua kadhaa za kurejesha uhusiano mzuri na wahisani.

No comments:

Post a Comment