TANGAZO


Monday, January 14, 2013

Mkutano wa Tathmini Mbio za Mwenge 2012, Mjini Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Zanzbar, Msham Abdulla Khamis, akifungua mkutano wa Tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2012,  kwa niaba ya Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Zainab Omar Mohammed leo, mjini Zanzibar. Mkutano huo umewashirikisha viongozi na waratibu wa mbio za mwenge kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar. (Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO)
Mwenyekiti wa mkutano wa tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2012, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga, akiongoza mkutano huo leo, mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Ali Nassoro Lufunga, Mkoa ambao ulikua mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka 2012.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Tathmini ya Mbio za Mwenge mwaka 2012, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano huo, kuhusu mafanikio, changamoto na namna ya kufanikisha shughuli za mbio za Mwenge nchini.
Mratibu wa Mbio za Mwenge mkoa wa Iringa, Atilio Mganwa akitoa mchango wake, kuhusu uboreshaji wa shughuli za Mbio za Mwenge nchini ambapo Mkoa wa Iringa utakuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa Mwaka 2013.
Washiriki wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaoendelea mjini Zanzbar.

No comments:

Post a Comment