Wanajeshi wa Ufaransa, wanasema kuwa wamefanikiwa kuingia katika mji wa waasi wa Kidal, ambao ndio ngome ya mwisho ya wapiganaji hao.
Huu ndio mji wa mwisho mkubwa ambao walilenga kuukomboa kutoka mikononi mwa wapiganaji.
Wanajeshi wa Ufaransa sasa wanadhibiti uwanja wa ndege wa Kidal, baada ya ndeghe zao pamoja na helikopta kutua huko usiku wa kumakial leo.
Wapiganaji wa kiisilamu waliriarifiwa tayari kuondoka mji humo na sasa ni wazi kuwa wanajeshi nduio wanaudhibiti.
Majeshi ya Mali na Ufaransa yamekuwa yakiwasaka waasi hao katima maeneo ya Kaskazini na hata kukomboa miji ya Gao na Timbuktu bila ya upinzani wowote.
Ufaransa ambayo ni koloni ya zamani ya Mali, ilianza harakati za kijeshi mwezi huu baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuonekana kuwa tisho kubwa katika maeneo ya Kusini.
'Kuangamiza Ugaidi'
Msemaji wa jeshi la Ufaransa kanali, Thierry Burkhard alithibitisha kuwa wanjeshi wa Ufaransa walishika doria katika eneo la Kidal usiku kucha Kidal".
Rais wa mpito wa jimbo la Kidal, Haminy Maiga, aliambia vyombo vya habari kuwa wanjeshi wa Ufaransa waliwasili kwa ndege za kijeshi na waliweza kuukomboa mji huo bila makabiliano.
"wanajeshi hao wanashika doria kwa usaidizi wa helikopta''
Mji wa Kidal,ambao uko umbali wa kilomita 1,500 kaskazini mashariki mwa Bamako, hadi ulipokombol;ewa ulikuwa chini ya udhibiti wa kundi la wapiganaji wa Ansar Dine.
Wapiganaji hao walitoroka Timbuktu ingawa walifaya kitendo cha kulipiza kisasi kabla ya kuondoka.
Hata hivyo, vuguvugu la Islamic Movement of Azawad (IMA), ambalo hivi karibuni,lilijitenga na makundi mengine ya wapiganaji, sasa linadhibiti Kidal, ingawa wapiganaji wa Tuareg pia wanadai kuudhibiti mji huo.
No comments:
Post a Comment