
Wachezaji wa Livepool wakicheza na Leeds
Luke Varney aliifungia Leeds bao lake la kwanza kabla ya Ross McCormack,
kufunga la pili. Tottenham ambayo inashiriki katika ligi kuu ya Premier nayo
ikapata bao lake kupitia kwa mchezaji wake Clint Dempsey.
Katika mechi nyingine Chelsea, nusura iage mashindano hayo baada ya kulemewa na Bendford.
Hata hivyo Fernando Torres aliifungia Chelsea bao lake la pili na kuiepushia aibu kubwa.

Wachezaji wa Leeds
Liverpool vile vile, imeondolewa kwenye michuano hiyo ya FA, baada ya kunyukwa magoli 3-2 na Oldham, ambayo inashiriki katika ligi daraja ya kwanza.
Timu zingine za ligi kuu ambazo zimefuzu kwa raundi ijayo ni pamoja na Manchester United, Everton, Arsenal, Wigan, reading na Manchester City.
Norwich, QPR na stoke city zinaungana na timu ambazo zimefunganya virago vyao katika michuano hiyo ya FA.
No comments:
Post a Comment