|
Na Magreth Magosso,Kigoma
ZAIDI ya abiria 25 wamenusurika kufa, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kutoka
Kigoma kuelekea Dar es Salaam kupata hitilafu ikiwa angani, jambo
lililomlazimu rubani wa ndege hiyo kuirudisha tena mkoani Kigoma.
Hali hiyo, imetokana jana saa kumi jioni, ambapo moja ya
vioo vya mbele ya ndege hiyo kilipasuaka na hivyo kuruhusu upepo mkali kuingia
ndani na kuwafanya marubani wa ndege hiyo, kufanya kazi ya ziada
kuhakikisha ndege, inatua salama katika Kiwanja cha ndege Kigoma.
Ndege hiyo ilikuwa katika safari yake ya kwanza kwa mwaka
huu, mkoani humo, ikiwa ni zaidi ya miezi 10 baada ya ndege nyingine
ya shirika hilo, kuanguka na mabaki yake kutelekezwa katika kiwanja cha ndege
kigoma huku sintofahamu ya kuondolewa kwa mabaki hayo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya abiria waliokuwemo
kwenye ndege hiyo Athumani Batumwa na Fred Mbassa walisema ndege hiyo inauwezo
wa kubeba abiria 50 ambapo ilipata itilafu baada ya dakika 30 kuanza kuruka kwa
chombo hicho kutoka kwenye uwanja wa ndege kigoma.
Kaimu meneja wa shirila la ATCL, Kepten Milton Lazaro
amekiri kutokea kwa itilafu hiyo na amewaondoa hofu wadau wa usafiri
huo, juu ta tatizo hilo na kwamba ni sehemu ya matatizo yanayoweza kutokea
kwa ndege yoyote.
Alisema kuwa utaratibu unafanywa kuhakikisha kwamba abiria
waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo wanatafutiwa ndege nyingine na kwamba hadi
kufikia leo abiria hao watakuwa wameshatafutiwa ufumbuzi lakini pia ndege hiyo
inaweza kuanza kufanyiwa marekebisho kuanzia baada ya kuwasili kwa spea.
|
No comments:
Post a Comment