Kwa Hisani ya Bin Zubeiry Blog
BONDIA Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ amefanikiwa kutetea taji lake la WBF uzito wa Bantam, baada ya kumpiga Nassib Ramadhan kwa Techinical Knockout (TKO) ya raundi ya 10 kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Temeke mjini Dar es Salaam usiku huu huku akishuhudiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk, Fenella Mukangala.
Nassib alionekana kuishiwa pumzi tangu raundi ya nane, lakini alijikongoja kutaka kumaliza raundi 12 za pambano hilo, ila kwa bahati mbaya, safari ikaishia raundi ya 10.
Hata hivyo, Nassib bondia kutoka Mabibo, jijini Dar es Salaam, alilianza vizuri pambano hilo akimsukumia mpinzani wake makonde mazito yaliyoonekana kumyumbisha.
Naasib aliendelea kutawala pambano hilo hadi raundi ya sita, baada ya hapo, mwelekeo wa pambano ulianza kubadilika taratibu, Chichi, mtoto wa Kinondoni akianza kumuadhibu mpinzani wake kwa makonde yake yaliyoshiba uzito.
Nassib alijitahidi mara moja moja kujibu mapigo, lakini zaidi alitumia ujanja wa kumkumbatia Chichi ili kumpunguza kasi.
Hata hivyo, Nassib hakushindwa kwa kupigwa ngumi, bali aliishiwa pumzi jambo ambalo linaashiria kijana huyo ni bondia imara na anaweza kuwa mpinzani wa kweli wa Chichi Mawe.
Kwa ujumla lilikuwa pambano zuri ambalo kwa muda mrefu halijapatikana katika ardhi ya Tanzania- mabondia walikuwa wakipigana, hakukuwa na ujanja ujanja. Wote ni mafundi na mamia waliohudhuria pambano hilo, waliburudika kwa mchezo mzuri.
Katika mapambano ya awali, Deo Samuel alitoka sare na Freddy Sayuni, Mohamed Matumla alimpiga kwa Knockout (KO) raundi ya pili Deo Miyeyusho, Fadhil Majiha alimpiga kwa pointi Juma Fundi na Ibrahim Classic alimpiga kwa pointi Said Mbugi.
Mgeni rasmi, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alimvalisha mkanda wa ubingwa Miyeyusho baada ya pambano hilo, lililohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.
![]() |
| Mabondia wastaafu, Emmanuel Mlundwa (kulia) na Habib Kinyogoli, wakizungumza jambo kwenye mpambano huo. |
![]() |
| Mohamed Matumla akiwa amebebwa juu baada ya kushinda pambano lake na Deo Miyeyusho kwa KO raundi ya pili. |
![]() |
| Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (kulia), akifurahia jambo na Waziri Dk. Fenella Mukangala katika meza kuu. |
![]() |
| Kutoka kulia, ni Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu', Mzee Matumla na Benny Kisaka. |
![]() |
| King Miyeysho ukipenda muite Chichi Mawe, akinyanyuliwa juu na mashabiki wake baada ya kumtwanga kwa TKO, Nassib katika raundi ya 10. |
![]() |
| Nassib akiwa amebebwa kutolewa ulingoni baada ya kula kichapo kutoka kwa Miyeyusho cha TKO katika raundi hiyo. |
































No comments:
Post a Comment