TANGAZO


Monday, December 10, 2012

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea, Serikali yatangaza kutenga sh. bil. 1.5 kusaidia Vijana

 


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), Phillippe Poinsot akifungua rasmi Siku ya Kimataifa ya Kujitolea bila malipo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Disemba ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Volunteer Action Counts.’
 

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea, Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Venerose Mtenga akihutubia na kuwaasa vijana kufanya kazi kwa kujitolea bila kusubiri malipo. Mgeni huyo, amewaasa vijana kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea kwa sababu Serikali kupitia Wizara yake imetenga shilingi bilioni 1.5 kwenye mfuko maalaum wa Vijana ili kuwakopesha kwenye vikundi vidogo vidogo ili wajiunge na ujasiriamali na kujitoa katika umaskini.
 

Mshereheshaji wa Siku ya Kimataifa ya kujitolea, Austin Makani akijadiliana jambo na washiriki kuhusiana na umuhimu wa vijana kujitolea.
 

Mgeni rasmi, Venerose Mtenga (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Phillippe Poinsot (wa pili ) na Afisa Program wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitole (UNV), Stella Karegyesa wakifuatilia program zilizokuwa zikiendelea wakati wa maadhimisho hayo.
 

Pichani Juu na Chini baadhi ya wanafunzi wa Vyuo mbalimbali, wanachama wa UN Clubs na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kujitolea, wakiwa katika hafla hiyo.
 

Baadhi ya washiriki wakijadiliana kuhusu umuhimu wa kujitolea katika makundi.
 

Mgeni rasmi, Venerose Mtenga na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP  Phillippe Poinsot (kushoto), wakitoka ukumbi.
 
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea, Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Venerose Mtenga, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), Phillippe Poinsot na Ofisa Program wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitole (UNV), Stella Karegyesa wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wakati wa hafla hiyo. (Picha na www.dewjiblog.com)

No comments:

Post a Comment