Mkuu wa Wialaya ya Ilala, Raymond Mushi akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi duka la vifaa vya ujenzi la Kampuni ya Nabaki Afrika lililopo makutano ya mitaa ya Kiungani na Sikukuu Kariakoo jijini Dar es Salaam leo, ambapo vifaa mbalimbali vya ujenzi vinapatikana. Kulia ni Mkurugenzi, Tania Hamilton na katikati ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamish Hamilton.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamish Hamilton, akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi moja ya vifaa vya ujenzi vinavyopatikana katika duka hilo, mara baada ya ufunguzi rasmi wa duka hilo leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamish Hamilton, akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Ilala moja ya mabati yanayopatikana katika duka hilo na kumueleza juu ya ubora wake, wakati akitembelea duka hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamish Hamilton, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakati wa uzinduzi wa duka la kampuni hiyo, ililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamish Hamilton, akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi mara baada ya kuwasili dukani hapo kwa ajili ya uzinduzi rasmi uliofanyika leo, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Huu ndiyo mwonekano wa duka la Nabaki Afrika lililopo Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
Jengo ambalo duka la Nabaki Afrika linapatikana, ambalo lipo katika makutano ya mitaa ya Kiungani na Sikukuu Kariakoo jijini Dar es Salaam linavyoonekana.
Nabaki Afrika imefungua rasmi tawi Kariakoo, katika eneo muhimu kibiashara, jiji la Dar-es-Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, amekata utepe na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamish Hamilton ameelezea kwamba Nabaki Afrika ipo katika kupanuka/kukua na hiyo imepelekea ufunguaji wa matawi jijini Arusha na hivi karibuni Mtwara.
Kwa ujumla Nabaki Afrika ina matawi manne jijini Dar-es-Salaam: Makao Makuu Mikocheni na matawi yaliyopo Mbezi beach, Masaki na sasa Kariakoo.
Kwa jinsi hii, Nabaki Afrika imeweza kuyafanyia kazi maombi ya wateja ya kurahisisha upatikanaji wa bidhaa bora za ujenzi.
"Wateja wetu wanahitaji bidhaa halisi na zenye ubora wa juu hivyo, ufunguaji wa matawi zaidi inarahisisha upatikanaji wa bidhaa hizi", alisema.
Tovuti mpya ya Kampuni hiyo, itapatikana hivi punde katika www.nabaki.com na bidhaa zote zitaweza kuonekana kupitia tovuti hii kwa mara ya kwanza. Kila bidhaa ina karatasi ya maelezo ambayo mteja anaweza kuipakua kutoka hapo. Hii itawasaidia wateja kuweza kupata taarifa muhimu ambazo zitawasaidia kufanya maamuzi juu ya bidhaa wanazohotaji.
Nabaki Afrika ina timu ya nje ya mauzo ambayo huenda katika soko kutafuta wateja wapya na pia kupanua Bohari ili kuweza kuhifadhi bidhaa nyingi zaidi.
Kila mwezi, karibu wateja wapya 5,000, hutembelea matawi ya Nabaki Afrika na kupokea mpaka barua pepe 10,000 na simu karibia 3,000.
"Tungependa kuwashukuru wateja wetu na waleta bidhaa wetu kwa ushirikiano wao na tunawatakia Heri ya krisimasi na mwaka mpya", alimaliza.








No comments:
Post a Comment