TANGAZO


Monday, December 31, 2012

Jambo Concepts wauaga mwaka 2012 City Sport & Lounge

 

Wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayotoa magazeti ya Jambo Leo, Dar Metro na Jarida la Jambo Brand wakichukua chakula, wakati walipokuwa wakisherehekea kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2013, kwenye mgahawa wa City Sports & Lounge, unaomilikiwa na kampuni hiyo juzi.

Wafanyakazi wa Jambo wakilainisha makoo kwa chakula safi na vinywaji kutoka mgahawa wa City Sports & Lounge.

Wafanyakazi wa Jambo wakila chakula safi kutoka mgahawa wa City Sports & Lounge.

Ilikuwa ni wakati wa maakuli, wafanyakazi wa Jambo wakijipatia chakula safi kutoka mgahawa wa City Sports & Lounge.

Wafanyakazi wa Jambo wakilainisha makoo kwa  chakula safi kutoka mgahawa wa City Sports & Lounge. Kulia ni Meneja Mkuu wa Jambo Concepts, Ramadhan Kibanike.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto), akiwa na mwandishi mwandamizi, Peter Ambilikile.
 
Wafanyakazi wa Jambo wakilainisha makoo kwa  chakula safi kutoka mgahawa wa City Sports & Lounge.

Meneja Mkuu wa Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Ramadhan Kibanike, akizungumza na wafanyakazi katika sherehe hiyo. 

Meneja Mkuu wa Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Ramadhan Kibanike, akimkabidhi mhariri wa jarida la Jambo Brand, Yakobe Chiwambo (kushoto), ambaye amekuwa mmoja wa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012, zawadi ya sh. 150,000.
 
Meneja Mkuu wa Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Ramadhan Kibanike, akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012, Amani Msyalha kutoka Idara ya Mauzo, zawadi ya sh. 150,000.
 
Meneja Mkuu wa Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Ramadhan Kibanike, akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012, Devota Akbar, wa Idara ya Mauzo, zawadi ya sh. 150,000.
 
Meneja Mkuu wa Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Ramadhan Kibanike, akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012, Nuru Abdallah kutoka Idara ya Utawala, zawadi ya sh. 150,000.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kulia), akimkabidhi zawadi ya mfanyakazi wa jumla, Dotto Mwaibale wa kitengo cha picha. Katikati ni Meneja Mkuu, Ramadhan Kibanike.
 
Julius Kihapa akiwa katika pozi na Mhasibu Mkuu, Vicky Mgoyo.
 
Hapa waandishi kutoka kushoto, Asma Mokiwa, Milka, Neema Mngonja na Asha Kigundula, wakifurahia na kuweka pozi la nguvu wakati wakipiga picha ya kumbukumbu katika sherehe hiyo. 
 
Waandishi hapa wakipata vinywaji huku wakitafakari, wakiwa na Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Anicetus Mwessa (wa pili kulia)
 
Joseph Mabulla akimkumbatia Neema Mngonja, wakati alipomfuata kwa ajili ya kufungua muziki katika sherehe hiyo. Anayefurahia kulia ni Asha Kigundula.
 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Concepts, Charity James, Asma Mokiwa na Grace Gurisha, wakipiga picha ya kumbukumbu.
 
Kinai na Clay wakitafakari kwenye sherehe hiyo.
 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Concepts, wakipiga picha ya kumbukumbu.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Concepts, wakipiga picha ya kumbukumbu.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto) na Meneja Mkuu, Ramadhan Kibanike, wakihesabu kura ya kumpata mfanyakazi bora wa jumla, ambapo mpigapicha Dotto Mwaibale aliibuka kidedea. Kulia ni Mhasibu Mkuu, Vicky Mgoyo.

Joseph Mabulla akizirudi ngoma na Neema Mngonja, wakati walipokuwa wakifungua muziki katika sherehe hiyo.
 
Baadhi ya wafanyakazi wakiserebuka na ngoma zilizokuwa zikiporomoshwa na Dj wa mgahawa wa City Sports & Lounge. 
 
Asha Kigundula akiwa na mumume, Majjid Mohamed katika hafla hiyo.
 
Joseph Mabulla hapa akizirudi ngoma na Charity James katika sherehe hiyo.
 
Hapa wafanyakazi wa Jambo Concepts, Julius Kihampa, akiwa amekishikilia kifaa chake, mama Grace Kingalame na Mama Asha Kigundula akiwa naye amemkumbatia, 
mumewe, Majjid Mohamed.
 
Wafanyakazi wa Jambo Concepts, Julius Kihampa, akiwa amekishikilia kifaa chake, mama Grace Kingalame na Mama Asha Kigundula akiwa naye amemkumbatia, mumewe,
 Majjid Mohamed.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Concepts, wakipiga picha ya kumbukumbu ya kuuaga mwaka 2012.
 

Wafanyakazi bora wakiwa katika picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (mwenye kofia), wakati wa sherehe hiyo.


No comments:

Post a Comment