TANGAZO


Tuesday, December 11, 2012

CRDB Bank yaingia Burundi

Jengo la Benki ya CRDB Burundi linavyoonekana.
Rais wa Burundi Piere Nkurunziza akiwasili katika sherehe za ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB jijini Bujumbura, Burundi. Benki ya CRDB imekuwa Benki ya kwanza ya kizalendo kufungua tawi lake nchini humo.
Rais wa Burundi, Piere Nkurunziza akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB nchini humo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Rais wa Burundi, Piere Nkurunziza akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa alipokuwa akiwasili katika sherehe hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi (kushoto) na Katibu wa Benki hiyo, John Rugambo (wa pili kushoto) na Meneja Mkuu wa Benki ya CRDB nchini Burundi, Bruce Mwile.
Rais wa Burundi, Piere Nkurunziza akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB nchini Burundi, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzao kutoka Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi huo. (Picha zote kwa hisani ya This Day Magazine)

No comments:

Post a Comment