TANGAZO


Wednesday, December 12, 2012

Balozi Sefue atambua mchango wa Luhanjo katika kujenga sekta binafsi

Na Mwandishi wetu
Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Balaza la Taifa la Biashara (TNBC), Balozi Ombeni Sefue, amesema uchumi wa Tanzania utaimarika vya kutosha kama wananchi wake watajenga ushirikiano thabiti na kuchukua hatua za kuondokana na hali duni ya ukuaji uchumi.
“Kama hatuwezi kushirikiana wenyewe basi hatutaweza kujenga nchi hata kama wafadhili wangetusaidia vipi. Ujenzi wa uchumi wa kweli wan chi hii upo mikononi mwa watanzania wenyewe,” alisema.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
Balozi Sefue alisema hayo katika hafla iliyoandaliwa kamati ya Baraza hilo ya Kumwaga Mwenyekiti mstaafu kamati ya utendaji, Mzee Phillemon Luhanjo ya jijini Dar es Salaam juzi usiku kwamba ushirikiano baana ya sekta za umma na binafsi ni muhimu sana katika kuchochea maendeleo ya uchumi.
“Tanzania ina raslimali nyingi, tukizisimamia vizuri na kuzitumia vyema tunaweza kujenga uchumi bora zaidi wa nchi yetu,” na kuongeza kuwa yeye kama Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji ya balaza atahakikisha sekta binafsi inafanya vizuri kwa ajili ya ukuaji wa uchumi.
Balozi Sefue alisema Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alijenga vitu vingi vikiwemo viwanda lakini vilianguka, hivyo jukumu lililopo ni kujenga misingi itakayosaidia uchumi kuimarika na nchi kujitegemea.
“Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji mstaafu ambaye piaKatibu Mkuu Kiongozi mstafu, Mzee Luhajo amefanya mengi ya kuimarisha mahusiano ya sekta Binafsi na Serikali kupitia TNBC, na mimi nitahakikisha ninadumisha mazuri yake yote kwa ajili ya kuendeleza uchumi wetu,” alisisitiza
Mwenyekiti Mwenza wa kamati ya utendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF),Bi. Esther Mkwizu alisema kiongozi huyo mstafu amefanya kazi kubwa ya kuijenga sekta binafsi na sasa taifa linanufaika na mchango wa sekta binafi katika uchumi wa nchi.
“Kuanzia mwaka 2001 kumekuwa na ushirikiano mkubwa kati ya sekta binafsi na umma kwa kufanya kazi kwa ubia ndiyo maana programu nyingi zimefanikiwa ikiwemo ya kilimo kwanza ambayo inazidi kushika kasi,”alifafanua Bi. Mkwizu.
Alimwomba mwenyekiti mpya wa kamati ya utendaji kufuata nyayo za mstafu huyo aliyejenga mazingira hayo ili kuhakikisha mahusiano hayo yanazidi kudumu ili sekta binafsi izidi kuwa injini ya kukuza uchumi.
Kwa upande wake, Mzee Luhanjo alisema sekta binafsi inaendelea vizuri tofauti na wakati alipokuwa anaingia katika nafasi hiyo aliyostafu nayo.
“Katika kuhakikisha sekta binafsi inazidi kufanya vizuri zaidi, watumishi wa serikali wanatakiwa kubadili tabia na kuwaona wawekezaji kuwa siyo wezi bali ni kiungo kikubwa cha uchumi wa nchi,”.
Alieleza kuwa sera na sheria za nchi ziwezeshe sekta binafsi kustawi kwa vile bila uwekezaji nchi haiwezi kutumia raslimali zilizopo kwa ajili ya ukuzaji pato la taifa, kuondoa umaskini na utoaji wa ajira kwa wananchi.
Alifafanua kuwa Tanzania haitakiwi kutegemea fedha za wafadhili bali mazingira yajengwe hapa nchini ya serikali na sekta binafsi kuendeleza miradi ya maendeleo.
“Nawashukururu wadau mbalimbali kwa kutambua mchango wangu kama mtumishi wa umma na zawadi mlizonipatia,” na kuongeza kusema sasa amerudi nyumbani kwake Njombe Iringa na kujihusissha na kilimo.

No comments:

Post a Comment