TANGAZO


Saturday, November 3, 2012

Mwanafunzi wa Jamaica ateswa na walinzi

Chuo kikuu kimoja nchini Jamaica kimeanza uchunguzi baada ya filamu iliyoonyesha mtu anayedaiwa kushiriki katika mapenzi ya jinsia moja akipigwa na walinzi waliowekwa kumlinda dhidi ya umati wa wanafunzi.

 
KIngston, Jamaica

Filamu hiyo inaonyesha mtu huyo akipigwa na walinzi katika chuo cha teknolojia cha mjini Kingston, ambapo alikimbizwa na umati wa watu waliokuwa wakimtukana.
Chuo hicho kimelaani kitendo hicho na kampuni ya ulinzi iliyowaajiri walinzi hao, imewafuta kazi.
Sheria ya Jamaica hairuhusu mapenzi ya jinsia moja.

No comments:

Post a Comment