TANGAZO


Saturday, November 24, 2012

Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal awasili Katavi kuzindua Uwanja wa ndege wa Mpanda na kongamano la tathmini ya Uwekezaji ukanda wa Ziwa Tanganyika

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal na mkewe, mama Aisha Bilal wakishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoani Katavi kwa ajili ya uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi, unaofanyika mjini mpanda kesho, Makamu wa Rais pia amezindua Uwanja wa ndege wa Mpanda na kuzindua Kongamano la Tathimini ya Mkutano wa Uwekezaji, Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana na kushirikisha Mikoa mitatu ya Rukwa, Kigoma na kufanyika mjini Mpanda ambapo sasa umekuwa Makao Makuu ya Mkoa wa Katavi.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Mpanda leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Rajab Rutenge na katikati ni mama Tunu Pinda.

 
Makamu wa Rais, Dkt Mohamed Gharib Bilal (kushoto), akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa Kongamano la kutathmini Mafanikio na Changamoto baada ya mkutano wa Uwekezaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika
uliofanyika  Kigoma na Rukwa uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana, mjini Mpanda.
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika uzinduzi wa Uwanja wa ndege wa Mpanda leo.  Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal na kulia ni mama Zakia Bilal.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza wakati wa uzinduzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo mchana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo,  akitoa taarifa ya ujenzi wa uwanja huo, kwa Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal wakati wa uzinduzi mjini Mpanda leo.
 
Ni aibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akimkaribisha Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal,  ili kuongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa uwanja huo mjini Mpanda leo.
 
 
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo. Kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Mama Zakia Bilal mke wa Makamu wa Rais.
 

Pichani Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye, Dk. Mary Nagu, Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Mke wa Waziri Mkuu na Mama Zakia Gharib Bilal, mke wake Makamu wa Rais wakiwa katika uzinduzi huo.
 
Makamu wa Rais akisalimiana na Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwekezaji mara baada ya kuwasili mjini Mpanda leo Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Katavi Mselem na kutoka kulia ni Mbunge wa Mpanda mjini CHADEMA Mh.Said Arfi na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk. Charles Tizeba.
 
Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mjini Mpanda mara baada ya kuwasili mkoani Katavi leo.
 
Makamu wa Rais akisalimiana akiwapungia mkono wananchi waliofika kumlaki kwenye Uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Dk. Rajab Rutenge na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa Bw. Mselem.
 
Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakia Bilal wakiangalia ngoma katika uwanja wa ndege wa Mpanda
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda akishiriki kuchza ngoma za asili za mkoa wa Katavi kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu.
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo na Mzee Paul Kimiti, Waziri Mkuu wa Zamani na Mbunge wa jimbo la Sumbawanga, miaka iliyopita kwenye uwanja wa ndege wa Mapanda.
 
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamoto wakati wa mapokezi hayo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutenge.
 
Waziri Mkuu Mizengo. akimpa ishara ya dole Mbunge wa Mpanda mjini CHADEMA Said Arfi, wakati wa mazungumzo yao kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda katika mapokezi ya Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal. Kauli mbiu ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Rajab Rutegwe katika maendeleo mkoani Katavi inasema “SIASA NI MAENDELEO”
 
Pichani kutoka kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injini Stella Manyanya, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dk. Rajab Rutenge, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Issa Machibya na Mwenyekiti wa CCM Mpanda, Hamida Mbogo wakizungumza mawili matatu wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais mjini Mpanda leo,


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mzee Chrisant Mzindakaya ambaye ni mwekezaji mkoani Rukwa na wawekezaji wengine kutoka India. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Rajab Rutenge.
 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Rajab Rutenge akizungumza katika kongamano hilo kwenye ukumbi wa Idara ya maji, mjini Mpanda na kukaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injini Stella Manyanya akizungumza na kutoa taarifa ya Mkoa wake katika suala zima la uwekezaji mkoani kwake.
 
Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Mary Nagu akizungumza katika kongamano hilo  baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, lililofanyika mjini Mpanda leo.
 
Mabalozi mbalimbali wamehudhuria katika sherehe hizo za uzinduzi wa mkoa wa Katavi kutoka Burundi, Zambia, Misri, Japan na DRC Kongo.
 
Waziri, Charles Tizeba akiwa na viongozi mbalimbali wa Vyama, Serikali na Taaisisikadhaa wamehudhuria katika kongamano hilo.
 
Baadhi ya wageni waliohudhuria kwenye uzinduzi wa mkuatno huo, wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais, Dk.  Bohamed Gharib Bilalal.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Issa Machibya akizungumza na kutoa taarifa ya Mkoa wake katika suala zima la uwekezaji mkoani kwake. (Picha zote na mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment