Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala watembelea Tume ya Mabadiliko ya Katiba jijini Dar
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia), akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, wakati wa ziara iliyofanywa na wajumbe hao leo, Jumanne Oktoba 16, 2012 ya kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika Makao Makuu ya Tume hiyo Jijiini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pindi Chana. (Picha zote na Tume ya Katiba)
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana (katikati), wakati wa ziara iliyofanywa na wajumbe hao leo, Jumanne Oktoba 16, 2012 na kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo Makao Makuu ya Tume hiyo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki.
Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Assa Rashid, akibadilishana mawazo na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, wakati wa ziara ya wajumbe hao, iliyofanywa leo, Jumanne Oktoba 16, 2012 na kutembela vitengo mbalimbali vilivyopo katika Makao Makuu ya Tume hiyo, jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni wajumbe wa Kamati hiyo, Rashid Ali Abdalla, Deogratius Ntukamazina, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na Felix Mkosamali.
No comments:
Post a Comment