Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya 67 ya Wiki ya Umoja wa Mataifa katika viwanja vya Karimjee leo, jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine amesisitiza juu ya umuhimu wa nchi za bara la Afrika kutathmini na kupima mafanikio ya malengo 8 ya millenia pamoja na kuongeza juhudi katika kupambana na umasikini na janga la njaa.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou akitoa salaam za Umoja wa Mataifa, wakati wa maadhimisho ya 67 ya umoja huo leo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwemo Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania, wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini, yaliyoongozwa na kauli mbiu ya uboreshaji wa maisha ya watu na uhifadhi endelevu wa mazingira kwa maisha bora leo, jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School), ambao walikuwa kivutio wakati wa maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, wakiwa katika gwaride maalum kupamba sherehe hizo.
Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School), wakiimba wimbo maalum uliobeba ujumbe wa kuhimiza utunzaji wa amani miongoni mwa Mataifa, wakati wa maadhimisho ya 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania leo, jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania, wakiimba wimbo uliobeba historia na mafanikio ya Umoja wa Mataifa, tangu kuanzishwa kwake leo, jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya 67 ya Wiki ya Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kupokea maelezo ya awali kutoka kwa Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), nchini Tanzania Hoyce Temu (kulia), kuhusu mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa rasmi kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na umoja huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini Tanzania.
Wadau wa kuhifadhi mazingira, wakionesha baiskeli za miguu miwili zisizotumia mafuta ambazo ni rafiki wa mazingira zenye uwezo wa kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine wakati wa maadhimisho ya 67 ya Wiki ya Umoja wa Mataifa leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO)









No comments:
Post a Comment