JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU
TAARIFA YA KAMATI NDOGO YA HAKI, KINGA NA MADARAKA YA BUNGE
Itakumbukwa kuwa wakati wa
Mkutano wa Nane wa Bunge uliofanyika kuanzia Juni – Agosti, 2012, Spika wa
Bunge aliunda Kamati Ndogo ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuchunguza
tuhuma zilizokuwepo kuwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na
baadhi ya Wabunge walijihusisha na Vitendo vya rushwa wakati wa mjadala wa
Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini (2012/2013).
Hivyo, Tangazo hili linatolewa
kuuarifu Umma kwamba Kamati hiyo Ndogo imekamilisha kazi yake kama
ilivyoelekezwa kwenye Hadidu za Rejea na kukabidhi Taarifa ya Uchunguzi huo kwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano tarehe 27 Septemba, 2012.
Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu
za Bunge (2007), Spika atatoa muongozo kuhusu utaratibu wa kufuata kuhusu
uwasilishaji wa Taarifa hii Bungeni ambapo yaweza kuwa Spika akatoa uamuzi ama
Kamati kuwasilisha Taaarifa hiyo Bungeni.
Spika atatoa taarifa ya
kukamilika kwa uchunguzi huo Bungeni wakati wa Mkutano wa Tisa wa Bunge
unaotarajia kuanza tarehe 30 Oktoba, 2012.
Imetolewa
na:
Ofisi
ya Bunge
S.L.P.
9133
DAR
ES SALAAM
No comments:
Post a Comment