TANGAZO


Saturday, October 27, 2012

Simba yailaza Azam FC mabao 3-1, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

 Aggrey Morris (13) wa Azam FC, akidhibiti mpira huku akiangaliwa na Emmanuel Okwi wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba imeichapa Azam mabao 3-1 katika mchezo huo. Anayeangalia katikati ni Salum Abubar wa Azam. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Emmanuel Okwi wa Simba akipambana na Salum Abubakar wa Azam FC, huku Jabir Aziz (kulia), akiangalia.

Emmanuel Okwi (katikati) wa Simba akijaribu kupita katikati ya Salum Abubakar (kushoto) na Jabir Aziz (kulia) wote wa Azam FC katika mchezo huo.


Emanule Okwi (kulia) wa Simba akiwania mpira na Agrey Moris wa Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


 Golikipa Ally Mwadini wa Azam FC, akimkata kwanja Mwinyi Kazimoto wa Simba katika kuondoa hatari langoni kwake wakati wa mpambano huo.


Wachezaji wa Simaba wakimpongeza Emmanuel Okwi (25) baada ya kufunga goli la pili kwa kichwa na kufanya mabao kuwa 2-1 wakati huo kabla ya kipindi cha pili cha mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


Wachezaji wa Simaba wakishangilia goli la pili la timu hiyo, lililofungwa na Emmanuel Okwi (25) kwa kichwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


 Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo.


 Mashabiki wa Azam FC, wakifuatilia mchezo huo.

Hadi kipind cha kwanza kinamalizika, matokeo yalikuwa kama yanavyoonekana kwenye ubao wa matangazo, Simba 2, Azam FC 1.


 Mrisho Ngassa wa Simba, akijaribu kumpiga chenga Sahim Nuhu wa Azam FC katika mchezo huo.


 Mrisho Ngassa wa Simba, akimtoka Sahim Nuhu wa Azam FC katika mchezo huo.


 Emmanuel Okwi (mbele), Felix Sunzu (katikati) na Amri Kiemba wakishangilia goli la 3 lililofungwa na shuti la juu na Okwi.


 Mchezaji Abdulham Humud (kulia) wa Azam FC, akiruka juu kuupiga kichwa mpita huku akiangaliwa na Sadi Morad wa timu hiyo na Amri Kiemba (kushoto) wa Simba.


Nassor Masoud 'Cholo' wa Simba akijaribu kumpiga chenga Agrey Morris wa Azam FC.



Nassor Masoud 'Cholo' wa Simba akipiga krosi mbele ya Agrey Morris wa Azam FC.

Hadi mwisho wa mchezo huo, matokeo yalikuwa kama yanavyoonekana kwenye ubao wa matangazo, Simba 3, Azam FC 1.

No comments:

Post a Comment