TANGAZO


Saturday, October 20, 2012

Sherehe za Mahafali Shule ya Sekondari ya Al Haramaini, Dar es Salaam zafana

Wanafunzi wa kidato cha Pili wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Aisha Kamna (wa pili kulia) na Nasra Mohamed (wa pili kushoto), wakisoma utenzi wakati wa sherehe za mahafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo, Dar es Salaam leo mchana. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, wakiwa kwenye mahafali yao ya 24 ya shule hiyo jijini Dar es Salaam leo mchana.


Baadhi ya wahitimu hao wa kidato cha nne wa Shule hiyo, wakiwa kwenye mahafali yao ya 24 ya shule hiyo, jijini Dar es Salaam leo mchana.




Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wa Shule hiyo, wakiwa kwenye mahafali yao ya 24 ya shule hiyo, jijini Dar es Salaam leo mchana.


Wanafunzi wa kidato cha Pili wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, wakisoma kaswida, wakati wa sherehe za mahafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo, Dar es Salaam leo mchana. 

Wanafunzi wakipiga dufu, wakati wa sherehe hizo, shuleni hapo leo mchana.

Mkuu wa Idara ya Sayansi wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwalimu Ramadhan Msuya, akiwaongoza wanafunzi Nazia Ibrahim (katikati) na Nuru Jabir, waliokuwa wakifanya zoezi la kuzalisha gesi ya Hydrogen na Oxgen, wakati wa sherehe za mahafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo, leo mchana.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Nuhu Jabir Mruma, akisoma risala ya shule hiyo, wakati wa sherehe za mahafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo, zilizofanyika kwenye viwanja vya shuleni leo mchana. Katikati ni mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Shule hiyo, Vyuo visivyo vya Kiserikali Tanzania ambaye pia ni Mjumbe Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mahmoud Mringo na kushoto ni Mwalimu wa Taaluma, Rashid Kassim.

Mgeni rasmi katika mahafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Shule hiyo, Vyuo visivyo vya Kiserikali Tanzania ambaye pia ni Mjumbe Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mahmoud Mringo, akitoa hotuba yake wakati wa sherehe hizo leo mchana. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Nuhu Jabir na kushoto ni Mwalimu wa Taaluma, Rashid Kassim.

Mwanafunzi bora wa pili wa Somo la Kiingereza kwa wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Bakari Ally Mohamed, ambaye pia alishinda katika somo la Physics, akipokea moja ya cheti chake kutoka kwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Shule hiyo, Vyuo visivyo vya Kiserikali Tanzania ambaye pia ni Mjumbe Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mahmoud Mringo.

Mhitimu Aisha Athumani akipokea cheti chake cha kumaliza kidato cha nne kutoka kwa mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Shule hiyo, Vyuo visivyo vya Kiserikali Tanzania ambaye pia ni Mjumbe Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mahmoud Mringo.



Mhitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Said Hajji Shah (kulia), akipokea zawadi kutoka kwa kaka yake, Yussuf Suleiman, mara baada ya kutunukiwa cheti chake cha kumaliza shule na mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Shule hiyo, Vyuo visivyo vya Kiserikali Tanzania ambaye pia ni Mjumbe Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mahmoud Mringo (hayupo pichani), shuleni hapo leo.

Mhitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Amina Ibrahim (wa tatu kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa ndugu, jamaa pamoja na familia yake, waliofika kwenye mahafali hayo, shuleni hapo leo mchana.

Wazazi, ndugu na jamaa za wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, wakiwazawadia zawadi mbalimbali pamoja na kuwavalisha mashada ya mau watoto na ndugu zao waliokuwa wakihitimu kidato cha nne shuleni hapo leo.

Mhitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Maimuna Abdul (kulia), akipewa zawadi na mama yake, wakati wa mahafali hayo, shuleni hapo leo mchana.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Nuhu Jabir Mruma, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali, wakati wa sherehe za mahafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo, kwenye viwanja vya shule leo mchana.


Mgeni rasmi katika mahafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Shule hiyo, Vyuo visivyo vya Kiserikali Tanzania ambaye pia ni Mjumbe Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mahmoud Mringo (katikati mwenye tai), akipiga picha ya pamoja na wahitimu wa kike wa kidato cha nne pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Nuhu Jabir (kulia kwa mgeni rasmi), mwishoni mwa sherehe za mahafali hayo.



Mgeni rasmi katika mahafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Shule hiyo, Vyuo visivyo vya Kiserikali Tanzania ambaye pia ni Mjumbe Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mahmoud Mringo (katikati mwenye tai), akipiga picha ya pamoja na wahitimu wa kiume wa kidato cha nne pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Nuhu Jabir (kulia kwa mgeni rasmi), mwishoni mwa sherehe za mahafali hayo.

No comments:

Post a Comment