TANGAZO


Tuesday, October 30, 2012

Maofisa Wakuu, Waandamizi wa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani mafunzoni nchini Ujerumani






















Mmoja wa Maofisa wa Polisi wa Ujerumani, akielekeza jambo kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga (watatu kushoto), ACP Kilonzo kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi (mwenye miwani) pamoja na ASP Msuyale (wa tatu mstari wa nyuma), wote kutoka nchini Tanzania, kuhusiana na mambo ya usalama barabarani wakati wakiwa katika ziara ya kimafunzo nchini Ujerumani.

Maofisa hao Wakuu, Waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka nchini Tanzania, walikuwa nchini Ujerumani kwa ziara ya mafunzo ya wiki moja (21/10 – 27/10/20120) katika Jimbo la Lower Saxon, ambapo pia walitembelea Mji Mkuu wa jimbo hilo, Hannover, Neunberg, na Gottingen. 

Aidha, ziara hiyo, ilihusisha mambo mbalimbali ya Usalama Barabarani, ikiwemo kuangalia upimaji mwendo kasi kwa kutumia mtambo maalum, unaopiga picha na rader ya kawaida, ukaguzi wa malori ya mizigo na mambo mengine mengi.

Mmoja wa Maofisa wa Polisi (mwenyeji), akieleza jambo kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga, ACP Kilonzo pamoja na ASP Msuyale (wote watatu pichani katikati), namna ya matumizi  mbalimbali ya usalama barabarani.

Mmoja wa Maofisa wa Polisi wa Ujerumani, akimuelekeza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga, namna ya kuangalia upimaji mwendo kasi kwa kutumia mtambo maalum unaopiga picha kuhusiana na uendeshaji magari barabarani.

Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga, ACP Kilonzo pamoja na ASP Msuyale, wakielekezwa namna ya leseni za madereva zinavyokuwa. 

Maofisa wa juu kutoka Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga, ACP Kilonzo pamoja na ASP Msuyale (wote watatu pichani mbele), wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao. (Picha zote kwa hisani ya SACP Mohammed Mpinga – CO Traffic)

No comments:

Post a Comment