TANGAZO

Tuesday, October 30, 2012

MamaTunu Pinda afungua Tamasha la Maonesho ya Wanawake wajasiriamali (MOWE), Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Tamasha la Maonesho ya Wanawake Wajasiriamali (MOWE), Elihaika Mrema akizungumza na kisha kumkaribisha Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (wa pili kulia), kufungua Tamasha la Maonesho hayo, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo, ambapo pia Mama Tunu Pinda, alizindua mradi wa Ujasiriamali wa Wanawake katika Kuwaendeleza na Kuwawezesha Kiuchumi (WEDEE) kwa mwaka 2012-2014, viwanjani hapo leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda vidogo na Biashara ndogo (SME), Dk. Consolotha Ishebali kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda vidogo na Biashara ndogo (SME), Dk. Consolotha Ishebali kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, akizungumza katika hafla ya kulifungua Tamasha la Maonesho ya Wanawake wajasiriamali (MOWE), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda, aliyelifungua tamasha hilo.

Baadhi ya Wanawake wajasiriamali, wakiwa kwenye ufunguzi wa Tamasha la Maonesho ya Wanawake wajasiriamali (MOWE), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka katika uzinduzi huo.

Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (kushoto), akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda vidogo na Biashara ndogo (SME), Dk. Consolotha Ishebali kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara (kulia), wakicheza wimbo maarufu wa msanii Vicky Kamata, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Wanawake Wajasiriamali na uzinduzi wa mradi wa Ujasiriamali wa Wanawake katika Kuwaendeleza na Kuwawezesha Kiuchumi (WEDEE) kwa mwaka 2012-2014, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda, akizungumza wakati alipokuwa akilifungua Tamasha la Maonesho ya Wanawake wajasiriamali (MOWE), Dar es Salaam leo, ambapo pia alizindua mradi wa Ujasiriamali wa Wanawake katika Kuwaendeleza na Kuwawezesha Kiuchumi (WEDEE) kwa mwaka 2012-2014.
 
Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda, akikata utepe ili kuzindua mradi wa Ujasiriamali wa Wanawake katika Kuwaendeleza na Kuwawezesha Kiuchumi (WEDEE) kwa mwaka 2012-2014, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam wakati alipokuwa akilifungua Tamasha la Maonesho ya Wanawake wajasiriamali (MOWE) leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa maonesho hayo, Elihaika Mrema na kulia Mshauri Mkuu wa mambo ya kiufundi kwa vijana kwa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, Jealous Chirove.

Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda, akifunua baadhi ya vijarida alivyokabidhiwa na wawakilishi wa UN nchini, ambao ni wadhamini wa maonesho hayo, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.

Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (wa pili kulia) pamoja na baadhi ya wanawake wakicheza wimbo maarufu wa Wanawake na Maendeleo wa msanii Vicky Kamata, wakati alipolifungua Tamasha la Maonesho ya Wajasiriamali wanawake (MOWE) na kuzindua mradi wa Ujasiriamali wa Wanawake katika Kuwaendeleza na Kuwawezesha Kiuchumi (WEDEE) kwa mwaka 2012-2014, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.

Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda, akiangalia nguo za kazi za wajasiriamali wanawake, mara baada ya kulifungua Tamasha la Maonesho ya Wanawake wajasiriamali (MOWE), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo, ambapo pia alikata utepe kwa ajili ya kuzindua mradi wa Ujasiriamali wa Wanawake katika Kuwaendeleza na Kuwawezesha Kiuchumi (WEDEE) kwa mwaka 2012-2014, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Biashara wa Kampuni ya Fruitful Gosheni, Pendo Eliya akimweleza jambo mama Tunu Pinda kuhusu bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo. Katikati ni Meneja Mtendaji wa Kampuni ya HOME Tanzania, Ekinala Kapusya.

No comments:

Post a Comment