TANGAZO


Thursday, October 11, 2012

Makamu wa Rais Dk. Bilal aomboleza kifo cha mfanyakazi wa Ofisi yake

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, Jenkins Chochole Matulile, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani kwao, Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam leo, Oktoba 11, 2012.  (Picha zote na OMR)
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Mama Mzazi wa marehemu, Jenkins Chochole Matulile, wakati alipofika nyumbani kwao kutoa pole na heshima za mwisho kutokana na msiba huo, wa aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifnyika nyumbani kwao Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 11, 2012.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Jenkins Chochole Matulile, aliyekuwa mfanyakazi katika Ofisi yake ya jijini Dar es Salaam, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani kwao, Mbezi Tangi Bovu na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 11, 2012.



No comments:

Post a Comment