TANGAZO


Monday, October 15, 2012

Makamu wa Rais Dk. Bilal afungua Mkutano wa kwanza wa Kimataifa barani Afrika wa kutangaza utalii wa nchi za Afrika

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipofungua Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo.  Mkutano huo umefunguliwa leo, Oktoba 15, 2012 katika Ukumbi wa AICC, Jijini Arusha na kuhudhuriwa na Mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika. (Picha zote na OMR)


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipofungua Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo.  Mkutano huo umefunguliwa leo, Oktoba 15, 2012 katika Ukumbi wa AICC, Jijini Arusha na kuhudhuriwa na Mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), akipokea barua ya wazi kutoka kwa Katibu wa Mkuu wa Shirika la Utalii la Dunia, Taleb Rifai, iliyotolewa na Baraza la Waendesha Utalii Duniani (WTTC), mara baada ya kufungua Mkutano wa Kuhamasisha Utalii barani Afrika leo, Oktoba 15, 2012, jijini Arusha. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mawaziri 17, kutoka nchi mbalimbali za Afrika.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), akipokea barua ya wazi kutoka kwa Katibu wa Mkuu wa Shirika la Utalii la Dunia, Taleb Rifai, iliyotolewa na Baraza la Waendesha Utalii Duniani (WTTC), mara baada ya kufungua Mkutano wa Kuhamasisha Utalii barani Afrika leo, Oktoba 15, 2012, jijini Arusha. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mawaziri 17, kutoka nchi mbalimbali za Afrika.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wasanii wa ngoma ya asili wa kabila la Kimasai waliokuwa wakitumbuiza wakati akiondoka katika ukumbi wa mikutano wa AICC, jijini Arusha leo, Oktoba 15, 2012 baada ya kuufungua mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia paketi ya unga wa Ubuyu na kusikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Moringa Consultancy (TZ) Co Ltd, Christina  Ngoti, wakati Makamu alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho baada ya kuufungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefanyika leo, Oktoba 15, 2012 jijini Arusha.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Tiba za Asili, James Kangaa, wakati Makamu alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho, baada ya kuufungua mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefanyika leo, Oktoba 15, 2012 jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment