Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa na pikipiki zao wakipita maeneo ya Posta Mpya kuwasaka muumini wa dini ya Kiislamu waliokuwa wameandamana leo mchana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyekamatwa na kushtakiwa kwa kuchochea vurugu, wizi na kuharibu mali za watu ambaye alifikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana na kisha kunyimwa dhamana.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa wamewakamata baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa wameandamana leo mchana, kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda.
Wananchi pamoja na wanafunzi wakikimbia kukamatwa na askari waliokuwa wakiwatafuta waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa wameandamana leo mchana, kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Issa Ponda.
Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa kwenye magari yao kuwatafuta waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa wameandamana leo mchana, kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyekamatwa na kushtakiwa kwa kuchochea vurugu, wizi na kuharibu mali za watu ambaye alifikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana na kisha kunyimwa dhamana.
Viongozi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi, wakishauriana wakati walipokuwa wakiwatafuta waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa wameandamana leo mchana, kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyekamatwa na kushtakiwa kwa kuchochea vurugu, wizi na kuharibu mali za watu ambaye alifikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana na kisha kunyimwa dhamana.
Askari Kanzu na Mgambo wa Jiji wakiwa wamewakamata baadhi ya vijana waliowashuku kuandamana na Waislamu kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Askari Kanzu wakimpandishi kijana waliyemkamata mewakamata wakimshuku kuandamana na Waislamu kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Askari Mgambo akiwa amemkwida wananchi akimpeleka kwenye gari la Polisi kwa ajili ya kudhibitiwa na kisha kupelekwa katika kituo cha Polisi, kutokana na kushukiwa kuandamana na Waislamu kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Ponda Issa Ponda, jijini Dar es Salaam leo.
Askari Mgambo wakiwa wamewakamata wananchi, wakiwapeleka kwenye gari la Polisi kwa ajili ya kudhibitiwa na kisha kupelekwa katika kituo cha Polisi, kutokana na kushukiwa kuandamana na Waislamu kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Ponda Issa Ponda, jijini Dar es Salaam leo.
Askari Mgambo akimpeleka binti aliyemkamata kwenye gari la Polisi kwa ajili ya kudhibitiwa.
Mgambo wa jiji, akimpeleka kijana, mfanyabiashara ndogondogo (machinga) kwenye gari la Polisi kwa ajili ya kudhibitiwa na kisha kupelekwa kituoni.
Vijana wakiwa wamejikusanya kufuatilia sakata hilo, huku wakiwa na wasi wasi wa kukamatwa na askari hao.
Mwananchi akionesha sehemu aliyojeruhiwa na bomu la machozi baada ya kumparaza kiunoni wakati lilipopigwa kuelekea sehemu yake.
Gari la maji ya kuwasha (washawasha), likiwa tayari kuwashughulikiwa vijana wa Kiislamu waliokuwa wakiandamana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Askari Kanzu na Mgambo wa Jiji wakiwa wamewakamata baadhi ya vijana waliowashuku kuandamana na Waislamu leo mchana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa ndani ya Msikiti wa Idrissa, Kariakoo kujihami wasikamatwe na Polisi, Mgambo, Askari Kazu pamoja na Jeshi la Wananchi, waliokuwa wakipita mitaani kuwaska waumini wa dini hiyo, waliokuwa wameandamana leo mchana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao Sheikh Ponda Issa Ponda.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, wakiwa tayari kwenye gari lao, kuwatafuta waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa wameandamana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, wakigawana risasi za mabomu ya kutoa machozi, tayari kukabiliana na waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa wameandamana leo mchana, kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakitendeka kwenye zoezi hilo leo mchana.
Muumini wa Dini ya Kiislamu akiwa amedhibitiwa ndani ya gari la Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) |
Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU), wakijiandaa kumwingiza katika gari muumini wa Dini ya Kiislamu aliyekamatwa katika maeneo ya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leoPolisi wakifanya doria kwa kutumia Pikipiki, maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo. Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na na ulinzi wa Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika mitaa ya Kariakoo leo.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa kwenye gari lao huku wakiwa wameshikilia silaha zao tayari kabili vurugu za waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa wakinadmana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wao, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo leo mchana.
Magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yakiwa katika doria katika barabara ya Msimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka kuandamana. (Picha zote na Dotto Mwaibale, Francis Dande wa Habari Mseto)
No comments:
Post a Comment