TANGAZO


Tuesday, October 9, 2012

Benki ya NMB yatoa msaada madawati 50 kwa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam

  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge ya jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye madawati  50 yenye thamani ya sh. mil. 5, yaliyotolewa msaada na benki ya NMB na kukabidhiwa na Meneja wa tawi la NMB  Bank House, Leon Ngowi (hayupo pichani), jijini Dar es Salaam leo.
    Meneja wa benki ya NMB tawi la Bank House,  Leon Ngowi (kulia), akimkabidhi moja ya madawati 50, yaliyotolewa na benki hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Hadija Telela. Madawati hayo yamegharimu shilingi milioni 5. Wanaoshuhudia ni Meneja wa NMB tawi la Bank House, Huduma kwa Wateja Stephen Chavalla na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Christina Wambura.
Meneja wa benki ya NMB tawi la Bank House,  Leon Ngowi (katikati) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Hadija Telela (kushoto), wakiwa wamekaa kwenye madawati na wanafunzi wa shule hiyo, mara baada ya kuwakabidhi madawati 50 yenye thamani ya sh. mil. 5 jijini leo.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge, wakifurahia madawati 50 yenye thamani ya shilingi Milioni 5, waliyokabidhiwa na Meneja wa NMB, tawi la Bank House,  Leon Ngowi (hayupo pichani), jijini Dar es Salaam leo.
 Wanafunzi wa kike wa Shule ya Msingi Bunge,  wakibeba moja ya madawati 50, waliyokabidhiwa na Meneja wa NMB, tawi la Bank House, Leon Ngowi (hayupo pichani), madawati 50, yenye thamani ya shilingi milioni 5, yaliyotolewa kwa shule hiyo, Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge,  wakibeba moja ya madawati 50, waliyokabidhiwa na Meneja wa NMB, tawi la Bank House, Leon Ngowi (hayupo pichani), madawati 50, yenye thamani ya shilingi milioni 5, yaliyotolewa kwa shule hiyo, Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge, wakiimba ngonjera, wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati 50, yenye thamani ya shilingi milioni 5, yaliyotolewa na benki ya NMB tawi la Bank House jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment