TANGAZO


Saturday, October 27, 2012

Babylove ndiye REDD'S MISS TANZANIA TALENT 2012

Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga akifungua rasmi shindano la Miss Tanzania Talent Show usiku wa kuamkia leo Hoteli ya Girrafe Ocean View, iliyoko kandokando ya bahari yaHindi, jijini Dar es Salaam. Warembo wameonesha vipaji vyao mbele ya watazamaji na wapenzi wa masuala ya urembo na ambapo walichujwa na kupatikana warembo watano watakaonigia kwenye tano bora na kutangazwa rasmi kuingia kwenye shindano la Miss Tanzania, litakalofanyika Ubungo Plaza Novemba 3 mwaka huu Pichani katikati ni Mbunge wa Arusha mjini viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Catherin Magige na kulia ni  Mkurugeni wa Hoteli ya Girrafe Ocean View, Charles Bekon.
Mshindi wa Miss Tanzania Talent Show, Babylove Kalala akicheza na nyoka wakati wa shindano hilo, lililofanyika usiku wa kuamkia leo, Hoteli ya Girrafe Ocean View kandokando ya bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.Hawa  ndio walioingia tano bora ya shindano hilo, lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View, jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Hoteli ya Girrafe Ocean View Bwana Charles Bekon, akikaribisha wageni mbalimbali waliofika katika shindano hilo.Miss World Tanzania, Lisa Jensen (kulia), akiongoza majaji wa shindano hilo, usiku wa kuamkia leo, Hoteli ya Girrafe Ocean View, kuwapata warembo hao.Wadau mbalimbali waliohudhuria katika onesho hilo, wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo usiku wa kuamkia leo. Mdau chini ni matukio mbalimbali ya show hiyo, jionee mwenyewe mambo yaliyojiri kwenye hoteli hiyo, usiku wa kuamkia leo. Ilimuwa ni burudani tupu na ya kupendeza kama sio kustarehesha kutoka kushoto ni Fredy, David na Isack.
Noella akionesha kipaji chake
Warembo juu na chini wakionesha vipaji vyao mbalimbali katika kumpata Redd's Miss Talent 2012

No comments:

Post a Comment